1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HEILIGENDAMM:Afrika kupata dola bilioni 60 kupambana na Ukimwi

8 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBtf

Viongozi wa mataifa yaliyostawi kiviwanda ulimwenguni G8 wanaokutana mjini Heiligendamm wameafikiana kutoa msaada wa dola biloni 60 kupambana na Ukimwi ,malaria na magonjwa mengine yanayosababisha idadi kubwa ya vifo barani humo.

Kansela wa Ujerumani Bi Angela Merkel anatarajiwa kutangaza rasmi makubaliano hayo baada ya kukutana na viongozi wa mataifa sita ya Afrika.

Aidha viongozi hao wanatarajiwa kujadilia mustakabal wa Kosovo vilevile suala la mpango wa nuklia wa Iran.Umoja wa mataifa imewekea vikwazo Iran ambayo bado inashikilia kuwa itaendelea kurutubisha madini ya uranium.

Viongozi hao wanatarajiwa kuidhinisha vikwazo zaidi endapo Iran inaendelea na mpango wake wa nuklia.Hapo jana viongozi wa G8 waliafikiana kupunguza viwngo vya gesi za viwanda ili kujaribu kupunguza ongezeko la joto ulimwenguni.