1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Heilingendam. Waandamanaji wapungua.

7 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBu3

Waandamanaji walioko katika mkutano wa mataifa yenye utajiri mkubwa wa viwanda G8 wameanza kupunguza jazba. Kiasi cha waandamanaji 1,000 wamejikusanya kwa amani katika maeneo mawili karibu na uzio wa waya wenye urefu wa kilometa 12 ambao unazunguka eneo la mkutano huo.

Jana Jumatano, polisi walitumia mabomba ya maji kuwatawanya mamia ya waandamanaji ambao , kwa karibu siku nzima , walizifunga barabara kadha zinazoelekea katika eneo la mkutano huo.

Kiasi cha waandamanaji 10,000 walijikusanya nje ya eneo hilo la mkutano na kiasi wengine 140 walikamatwa.

Wakati huo huo katika kuadhimisha siku ya mkutano mkuu wa kanisa la kiinjili duniani mjini Kolon, wawakilishi wa dini nane duniani zilizoalikwa kuhudhuria mkutano huo wametoa wito kwa mkutano wa mataifa yenye viwanda duniani G8 kupambana na umasikini duniani.

Mwenyekiti wa baraza la ushauri la kanisa hilo Wolfgang Huber , amesisitiza upigaji marufuku biashara ya silaha pamoja na shughuli za kijeshi za mataifa hayo ya G8.