1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Helsinki. Chama cha waziri mkuu chashinda.

19 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCHZ

Chama cha mrengo wa kati cha waziri mkuu Matti Vanhanen kimekipata ushindi finyu katika uchaguzi mkuu wa bunge nchini Finland.

Lakini matokeo yaliyotolewa wakati kura zote zimekwisha hesabiwa zinaonyesha kuwa upande wa upinzani wa chama cha kihafidhina umepata ongezeko kubwa, kwa kuchukua viti 50.

Hii ni idadi ya kiti kimoja pungufu kuliko kilivyopata chama cha mrengo wa kati , na ni viti vitano zaidi kuliko kilivyopata chama cha Social Democrats, ambao ni washirika katika serikali ya mseto ya waziri mkuu Vanhanen.

Wachunguzi wa masuala ya kisiasa wanasema kuwa matokeo hayo yanaweza kusababisha kuundwa kwa serikali mpya ya mrengo wa kati kulia.