1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hertha yalenga kuipunguza kasi ya Bayern

19 Septemba 2016

Hertha Berlin ambayo imeanza msimu kwa kishindo itajaribu siku ya Jumatano kuiwekea breki Bayern Munich katika mchuano wa kusisimua wa timu hizo mbili zilizo kileleni mwa Bundesliga

https://p.dw.com/p/1K4vv
Fußball Bundesliga Hertha BSC - FC Schalke 04
Picha: Getty Images/Bongarts/B. Streubel

Ushindi wa Hertha wa maba mawili kwai sifuri nyumbani dhidi ya Schalke hapo jana una maana kuwa Berlin na Bayern, ni timu pekee za Ujerumani ambazo zinashikilia rekodi ya asilimia 100 kwa kupata ushindi mara tatu katika mechi tatu na zitakwaruzana katika uwanja wa Munich wa Allianz Arena.

Bayern inapaa paa lakini Hertha yake kocha Pal Dardai ni miongoni mwa timu zinazoonekana kuidhoofisha Bayern. Ushindi wa jana dhidi ya SCHALKE ulikuwa wa tatu katika mechi tatu. Huyu hapa kocha Dardai "Kwangu mimi, ilikuwa vizuri kwa sababu kila kitu kilikuwa sawa na tukaudhibiti mpira. Na kushinda dhidi ya timu kama Schalke na kudhibiti kila kitu, nadhani ni jambo zuri la kutufanya tujiamini. Na kupata pointi tisa kutokana na mechi tatu za kwanza ni kitu kizuri. Tunapaswa kuendelea kufanya kazi tu.

Kando na mchuano wa Bayern na Hertha, Borussia Dortmund ambao wamesajili ushindi wa 6 -0 mara mbili mfululizo dhidi ya Legia Warsaw na Darmstadt, watakuwa nyumbani kwa Wolfsburg kesho Jumanne. Kocha Thomas Tuchel ameonya wanapaswa kujiandaa kwa michuano mikali ijayo.

Deutschland Fußballtrainer Thomas Tuchel in Dortmund
Thomas Tuchel anasema Dortmund sasa wameimarikaPicha: picture alliance/abaca

Wolfsburg wamepata ushindi mmoja tu katika mechi zake tatu za ligi na wakatoka sare ya bila kufungana dhidi ya Cologne na Hoffenheim katika mechi zake mbili za mwisho. Schalke itakutana na Cologne siku ya Jumatano ikihitaji sana pointi tatu baada ya kupoteza mechi zake tatu mfululizo. Nayo Werder Bremen itachuana na Mainz.

Bremen ilimpiga kalamu kocha wake Viktor Skripnik hapo jana kufuatia kichapo chao cha mabao manne kwa moja dhidi ya Borussia Moenchengladbach. Kilikuwa kichapo chao cha nne mfululizo na mwanzo mbaya kabisa wa msimu katika historia ya klabu hiyo. Kocha wa Gladbach Andre Schubert anaeleza ni kwa nini matokeo hayo yalikuwa ya kuridhisha. "Nimeridhika, kwa sababu tulijaribu sana kuanzia dakika ya kwanza kuutawala mchezo, kumshambulia mpinzani mara moja na kuchukua mpira ili kujaribu kutumia nafasi zilizokuwapo kuelekea langoni. Vijana wangu wamecheza sasawa kabisa na wakatumia nafasi walizopata za kufunga mabao, na mwishowe tukafungwa bao lisilo la kawaida

Mechi nyingine za kesho ni: Freiburg v SV Hamburg, Darmstadt v Hoffenheim, Ingolstadt v Eintracht Frankfurt, wakati Jumatano, RB Leipzig v Borussia Moenchengladbach na Bayer Leverkusen v Augsburg

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA
Mhariri: Yusuf Saumu