1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kinyang'anyiro cha rais wa Marekani

Bergmann/Hamidou9 Januari 2008

Maajabu yazuka New-Hampshire,mbio za kuania tikiti ya Democratic ziwazi.

https://p.dw.com/p/Cmug
Mshindi wa New Hampshire Hilary ClintonPicha: AP Photo

Baada ya kushindwa Iowa na Barak Obama,nafasi ya Hilary Clinton ya kuibuka na ushindi katika kinyang'anyiro cha kuania nafasi ya kugombea kiti cha rais huko New Hampshire kwa tikiti ya chama cha Democratic ilionekana kua duni.Hasa kwakua utafiti wa maoni ya umma ulikua kila kwa mara ukiashiria atashindwa.Lakini Hilary Cliton amezusha maajabu.

Hilary amesharejea tena jukwaani.Licha ya matokeo mabaya ya kura za maoni ya umma za hivi karibuni yaliyoashiria angekua nyuma ya Barak Obama,senetor huyo wa New York amempita kidogo mpinzani wake,senetor wa Illinois, katika kinyang'anyiro cha kugombea nafasi ya kupigania wadhifa wa rais kwa tikiti ya chama cha Democratic Alionekena kama mtu aliyeshusha pumzi alipowahutubia wafuasi wake kuwashukuru:
"Kampeni hii ya uchaguzi itaibadilisha Marekani.Kwasababu tutakabiliana na changamoto zilizoko na tutaitumia fursa iliyoko.Sitokua hata siku moja peke yangu,nitafuatana na mamilioni kwa mamilioni ya watu,ambao wanaamini kama mimi,nchi hii inastahiki mtu kuipigania."
Hata Baraka Obama anaiangalia nagasi ya pili aliyojipatia New Hampshire kua ni ushindi.Anasema yuko tayari kuendelea na juhudi za kumaliza mgawanyiko.
"Kuna kinachotokea kama watu hawakipigii kura chama chao na badala yake wanapigia kura kwaajili ya matumaini ya pamoja.Kwasababu,tajiri au maskini,mweusi au mweupe,mlatino au muasia,Iowa au Hampshire,Nevada au South Caroline,sote tuko tayari kuipatia muongozo mpya nchi hii.Na haya ndio yanayojiri hivi sasa Marekani.Mageuzi ndio yanayotokea."
John Edwards,senetor wa zamani wa South Caroline amemaliza nafasi ya tatu.Kwa hivyo mashindano ya kugombesa wadhifa wa rais kwa tikiti ya chama cha Democratic bado yanaendelea.Barak Omaba hakufanikiwa kujivunia ushindi kama ule alioupata Iowa.Wakinamama safari hii wamemchagua Hilary Clinton..Na wapiga kura wasioelemea upande wowote wameelekea upande wa Republican na kumuunga mkono John McCain. Ushindi wake ulijitokeza tangu mwanzo.Kabla ya kuhesabiwa angalao asili mia 20 ya kura,vituo vya televisheni vilimtangaza Senetor huyo wa Arizona mwenye umri wa miaka 71 kua mshindi na wafuasi wake wakamshangiria."MacCain juu "
Mbinu za mwanasiasa huyo aliyepigana zamani vita vya Vietnam,anaeunga mkono vita vya Irak licha ya kukosoa mbinu zinazofuatwa Irak zimeleta tija.Katika hotuba yake,McCain ambae kampeni yake ilikua nusra ivunjike mwaka jana kutokana na ukosefu wa fedha,ameelezea azma ya kurekebisha makosa ya kisiasa ya miaka ya nyuma.Anasema
"Sijenda Washington kutetea masilahi yangu.Nimekwenda huko kuitumikia nchi yangu.Na hilo,marafiki zangu ndilo lenyewe hasa nitakalofanya,nikibahatika na kupata fursa ya kuchaguliwa kua rais wenu."
McCain amemshinda mpinzani wake Mitt Romney,gavana wa zamani wa Massachussets ambae kwa mara ya pili ameshindwa kujipatia ushindi.