1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hillary Clinton aihitimisha ziara ya Tanzania

13 Juni 2011

Waziri wa mambo ya nje wa marekani Bi Hillary Clinton amekamilisha ziara yake ya siku tatu nchini Tanzania akisifia mahusiano baina ya nchi hizo mbili lakini pia amejadilia pia hali ya mambo nchini Zimbabwe na Sudan.

https://p.dw.com/p/11ZN5
Hillary Rodham Clinton, Waziri wa mambo ya Nje wa MarekaniPicha: AP

 Bi Clinton, aliyewasili nchini Tanzania mwishoni mwa juma akitokea Lusaka, Zambia, amekuwa na majadiliano ya faragha na Rais Jakaya Kikwete na baadaye kukutana na waandishi wa habari ambako wote kwa pamoja wamezungumzia mkwamo wa kisiasa unavyojiri huko Zimbabwe na machafuko yanayoendelea sasa katika jimbo la Abyei, nchini Sudan.

Tansania USA Präsident George Bush Reise in Afrika Jakaya Kikwete
Rais Jakaya Kikwete na Rais George W Bush aliyeizuru Tanzania mwaka 2008Picha: AP

Usuhuba mzuri

Kabla ya kufikia hoja hiyo kwanza walijadiliana siasa za nchi mbili-yaani Tanzania na Marekani- ambako wakaeleza kuwa mataifa hayo yanaendelea kudumisha mahusiano yao na kuahidi kuongeza maingiliano zaidi kwenye sekta za uchumi na biashara.Rais Kikwete aliisifu Marekani namna inavyoendelea kutoa mchango kusaidia sekta za afya, elimu na maeneo mengine iikwemo ukuzaji uchumi na maendeleo

Amedai kuwa mashirikiano hayo yamesaidia pakubwa kusukuma mbeleo ustawi wa maisha na ukuzaji uchumi. Eneo alilolitaja kupata mafanikio makubwa ni juu ya mapambano ya ugonjwa wa Malaria ambako amesema hali ya ugonjwa huo imedhibitiwa vyakutosha.

Uchumi na Biashara

Hillary Rodham Clinton in Kongo Flash-Galerie
Hillary Rodham Clinton: Akiwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo mwaka 2009Picha: AP

Lakini pia viongozi hao wamejadiliana juu ya masuala ya uchumi na biashara. Katika miaka ya hivi karibuni hali ya ufanyaji biashara ya moja kwa moja baina ya mataifa hayo mawili imekuwa katika kiwango cha kurishisha, na wataalamu wa masuala ya uchumi wanaona kuwa ongezeko hilo linatazamiwa kuendelea kukaa zaidi

katika kipindi kijacho.

Kwa mwaka jana pekee, Marekani ilisafirisha bidhaa nchini Tanzania zinazofikia thamani ya dola milioni 164, wakati Tanzania ilifanikiwa kuvuna kiasa cha dola milioni 43 kutokana na bidhaa zake iliyosafirisha katika soko la Marekani.

Mchango wa kisiasa

Na katika siasa za kimataifa, Waziri huyu wa mambo ya nje amezihimiza nchi wanachama wa Jumuiya ya maendeleo kusini mwa Africa -SADC- kuongeza juhudi ili kutatua mkwamo wa kisiasa unaoikabili serikali ya umoja wa kitaifa ya Zimbabwe.

Alipogeukia hali ya mambo huko Sudan hasa katika jimbo la Abyei, ambako serikali ya Al Bashiri imepeleka vikosi vyake, Bi Clinton ametaka Khartoum kutambua kuwa inawajibu wa kusimamia mchakato wa ufikiaji amani kwa kufuata maridhiano yaliyofikia hapo kabla nataka iviondoshe vikosi vyake kwenye eneo hilo.

Präsident Jakaya Mrisho Kikwete
Rais Jakaya Mrisho KikwetePicha: AP Photo

Bi Clinton kwa hivi sasa ameelekea nchini Ethiopia ambako anatazamiwa kujadiliana na mwenyeji wake kuhusu siasa za Pembe ya Afrika.

Mwandishi: Njogopa, George

Mhariri: Othman,Miraji