1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hisia tofauti zatanda Uganda baada ya matokeo

21 Februari 2011

Nchini Uganda inaripotiwa hali ni ya hisia tafauti miongoni mwa wakaazi wake baada ya hapo jana rais Museveni kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa rais

https://p.dw.com/p/10LOJ
Wafuasi wa chama tawala NRM wakisherehekea mitaaniPicha: picture alliance/dpa

Mpinzani wake mkuu Kizza Besigye ameyakosoa matokeo hayo na kudai kwamba hana imani na mahakama kuu ya nchi hiyo hivyo basi anatafakari juu ya kuchukua hatua nyingine.Kizza Besigye amedai kwamba kumefanyika udanganyifu mkubwa katika zoezi zima la upigaji kura.Nini maoni ya walioko nje na Uganda kuhusu hali ilivyo.Nimezungumza na Salim Msoma mchambuzi wa masuala ya Kisiasa kutoka Tanzania na rafiki wa rais Yoweri Museveni na kwanza anaelezea hisia zake kuhusu ushindi wa Museveni.

Mwandishi,Saumu Mwasimba

Mhariri:AbdulRahman