1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Historia fupi ya mkutano wa mataifa yenye utajiri mkubwa wa viwanda G8.

Sekione Kitojo24 Mei 2007

Kuanzia mwaka 1975 wanakutana wakuu wa nchi na serikali wa mataifa tajiri yenye viwanda duniani kila mwaka katika mkutano wa kiuchumi, unaojulikana kama mkutano wa kundi la G8. Kutoka katika ushiriki wa wakuu sita wa nchi ambao walishiriki mkutano usio rasmi hivi leo kuna kundi la mataifa manane ambayo ni pamoja na Marekani, Ufaransa, Uingereza, Ujerumani, Japan , Italia na Russia. Rolf Wenkel anazungumzia historia ya mkutano huo

https://p.dw.com/p/CB3y
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel akilihutubia bunge la Ujerumani Bundestag, akifafanua kuhusu masuala ya G8.
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel akilihutubia bunge la Ujerumani Bundestag, akifafanua kuhusu masuala ya G8.Picha: AP

Mkutano wa kwanza wa kiuchumi duniani wa kundi hili uliitishwa kwa mara ya kwanza mwaka 1975 na ya rais wa zamani wa Ufaransa Valery Giscard d’Estaing na kansela wa zamani wa Ujerumani Helmut Schmidt , na viongozi sita wa mataifa ya Ujerumani, Ufaransa, Italia, Japan , Uingereza na Marekani wakakutana katika kasri la Rambouillet karibu na mji mkuu wa Ufaransa , Paris. Hapo viongozi hao walitaka siasa za kiuchumi za dunia wazijadili katika hali ya pamoja na yenye wepesi zaidi.

Mwaka mmoja baadaye , mjini Pueto Rico, Canada iliingizwa katika kundi hilo, la mataifa na kuwa kundi la mataifa saba G7.

Kwa Wajerumani wengi mkutano hususan wa mjini Munich mwaka 1992 ungeweza kubakia katika kumbukumbu yao, lakini sio hivyo, kwani ni katika mkutano huo ushirikiano mpya na Russia ulianzishwa. Yalifanyika mapambano makali ya polisi dhidi ya wale wanaopinga mkutano huo katika siku za mwanzo za mkutano huo nchini Ujerumani kutokana na tofauti kubwa ya mawazo juu ya polisi kutumia nguvu kupita kiasi maandamano .

Mwanzo mpya wa kisiasa ulionekana katika mkutano wa mwaka 1994 mjini Napoli katika siku ya mwisho. Kwanza rais wa Russia Boris Yeltsin alitambulika rasmi kama mhusika wa masuala ya ushauri wa kisiasa. Sasa rasmi ni kundi la mataifa manane G8, amesema kansela wa zamani wa Ujerumani Helmut Kohl.

Mwaka 1998 mjini Birmingham Russia ikawa rasmi nchi inayotambulika yenye umuhimu mkubwa kisiasa.

Kundi hilo lilikuwa likitarajia kwa hiyo kuwa kundi la G8.

Katika masuala ya siasa za uchumi na fedha yalikuwa yanakutana tu hata hivyo mataifa ya G7, wakati Russia kuhusiana na mada hii haiwezi kulingana na jukumu la mataifa haya ya G7 yanavyojihusisha na dunia.

Mkutano uliofanyika mjini Kolon Juni 1999 unaingia katika historia kuwa ni mkutano kuhusu madeni.

Mataifa masikini duniani yalisamehewa madeni yanayofikia Dola bilioni 70, na kufungua njia ya kuinua hali bora ya maisha.

Zaidi ya watu 50,000 walifanya maandamano mjini Koln na Stuttgart kudai kupunguzwa zaidi kwa madeni.

Mjini Genoa mkutano huo wa kiuchumi wa 27 katika mwaka 2001 , uliingia hali ya wasi wasi , kutokana na maandamano makubwa na uharibifu pamoja na matumizi makubwa ya nguvu ya polisi ambayo yamesababisha kuchukua nafasi kubwa katika vyombo vya habari na kusababisha mjadala mkubwa kuhusiana na tukio kama hilo la mkutano huo mkubwa.

Katika siku ya mwanzo tu mmoja kati ya waandamaji waliokuwa wakifanya ghasia alipigwa risasi na polisi. Watu 561 walijeruhiwa kutokana na ghasia hizo. Kiasi cha watu 300 wanaopambana dhidi ya utandawazi walikamatwa na polisi, kati ya hao Wajerumani 71. Kansela wa zamani Gerhard Schroeder akasema mwishoni mwa mkutano huo.

Kwa kweli hatuwezi kuruhusu, wawakilishi wa waandamanaji wanaofanya ghasia kutoka katika mataifa ya kidemokrasia , ikiwa vipi wanakutana, wachache ama mia kadhaa ama maelfu wakiwa tayari wameamua kufanya ghasia. Ndio sababu pia hakuna sababu ya kujiuliza , iwapo mikusanyiko hiyo inapaswa kuruhusiwa kutokea tena ama la.

Mkutano wa mwaka 2005 katika mji wa Scotland wa Gleneagles uligubikwa na wimbi la ugaidi mjini London. Katika siku ya pili ya mkutano huo kulitokea milipuko katika kituo cha ardhini cha treni na mabasi, milipuko ambayo imesababisha watu zaidi ya 50 kuuwawa, mamia wakiwa wamejeruhiwa.

Mwaka uliopita kulifanyika mkutano wa 32 wa kiuchumi katika mji wa Sant Petersburg. Mada kuu ikawa ni usalama wa nishati ya kinuklia, pamoja na hali ambayo si salama katika mashariki ya kati.

Katika sula hilo rais wa Russia Vladimir Putin na rais wa Marekani George W. Bush walionekana kutofautiana mno. Kansela wa Ujerumani Angela Merkel anaingia katika mkutano huo kwa mara ya kwanza.

Kwa kweli tumekuwa na hali, ya uwazi na kutokana na matatizo makubwa tuliyonayo, pia ulazima wa kupata msimamo wa pamoja , imekuwa kubwa zaidi.

Uzito wa kundi hili la G8 unapatikana pia katika hesabu kwani kundi hili linachangia kiasi cha theluthi mbili ya biashara yote inayofanyika duniani, na zinatoa kiasi cha robo tatu ya misaada ya maendeleo duniani na ndio zinachangia kwa kiasi kikubwa katika mashirika ya kimataifa kama vile katika shirika la fedha la kimataifa IMF na benki kuu ya dunia.