1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Sheria na HakiKimataifa

Hizi ndizo nchi zenye ufisadi mdogo zaidi duniani

30 Januari 2024

Kulingana na ripoti mpya ya shirika la kimataifa la kufuatilia masuala ya ufisadi la Transparency, Denmark, Finland, New Zealand na Norway ndizo nchi zilizo na ufisadi mdogo zaidi duniani.

https://p.dw.com/p/4bq1v
Chapa ya shirika la Kimataifa la Transparency
Chapa ya shirika la Kimataifa la Transparency ikionekana katika simu ya kiganjani Picha: Rafael Henrique/ZUMA Wire/IMAGO

Ripo hiyo mpya iliokwenda kwa jina la "Kielelezo cha Mtazamo wa Ufisadi," Ujerumani imesalia katika nafasi ya tisakatika viwango hivyo ambavyo vilitathmini watendaji, wataalam na taasisi kwa ujumla wake.

Chini ya orodha hiyo ni nchi zinazokumbwa na migogoro kama vile Syria, Venezuela na Somalia.

Mkuu wa shirika hilo Alexandra Herzog, amesema kwamba "pale ambapo utawala wa sheria, uhuru wa vyombo vya habari na mashirika ya kiraia yanapodhoofishwa, basi rushwa hutawala."

Soma pia:Museveni atimiza miaka 38 madarakani akililia ufisadi

Aidha mkuu huyo wa Transpancy Intarnational, ameitaja Hungari chini ya utawala wa Waziri Mkuu Viktor Orbán, imeshuka hadi nafasi ya 76, ikiwa ni nafasi mbaya zaidi kama taifa lililo ndani ya Umoja wa Ulaya.

"Uwajibikaji dhaifu na ufisadi wa kisiasa unadhoofisha utawala wa sheria katika eneo ambalo watu wanapoteza imani katika taasisi zao" Alisema.

Aliongeza kuwa katika matukio ya kutisha zaidi, makundi yenye maslahi madogo yana udhibiti mkubwa wa kufanya maamuzi ya kisiasa, na pengine serikali zinawalenga waandishi wa habari, watoa taarifa na waangalizi na wafuatiliaji wa mambo kwa ukaribu.

Nafasi ya Afrika inaridhisha katika ripoti hiyo?

Mataifa yalio Kusini mwa Jangwa la Sahara yamepata kiwango cha chini zaidi, licha ya baadhi ya nchi kufanya maboresho makubwakatika taasisi zake.

Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo | Rais Felix Tshisekedi.
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Felix TshisekediPicha: Isa Terli /AA/picture alliance

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Fedha IGF inalo jukumu muhimu katika juhudi za kupambana na rushwa chini ya Rais Felix Tshisekedi.

Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, IGF imefichua visa vingi vya ubadhirifu wa fedha za umma na ufisadi katika taasisi kadhaa za umma, ikiwa ni pamoja na ofisi ya rais.

Soma pia:Ufisadi Kenya: Mihimili mitatu ya serikali yapewa siku 30

Hata hivyo, haki imekuwa ikitendeka kwa mwendo wa kinyonga, hasa kwa kesi zinazohusu watu waliowekwa hadharani kupitia majukwaa ya kisiasa.

Wakati wa mahojiano mnamo Julai 2023, Rais Tshisekedi alionyesha kutoridhishwa na utendajikazi wa mahakamawakati wa uongozi wake wa muhula iliopita.

Ripoti hiyo ya kila mwaka ya Mtazamo wa Rushwa, inakusanya takwimu na matokeo kutoka taasisi 12 zinazojitegemea zilizobobea katika uchambuzi wa utawala na mazingira ya biashara.

Vyanzo vikijumuisha tafiti kutoka taasisi mbalimbali za kimataifa ikiwemo taasisi ya Ujerumani ya Bertelsmann, Benka ya Maendeleo ya Afrika.

Vita dhidi ya ufisadi michezoni Kenya