1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ho Chi Minh City, Watu kadha wauwawa na kimbunga.

5 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCmN

Kimbunga cha maeneo ya tropiki kinachojulikana kama Durian, kimesababisha watu 23 kupotea maisha kusini mwa Vietnam.

Kimbunga hicho kikiwa na upepo unaokwenda kilometa 120 kwa saa, kimelikumba eneo la bonde la jimbo la Mekong, ambako limesababisha uharibifu mkubwa.

Kisiwa cha Phu Quy, kilichoko kilometa 250 mashariki ya mji wa Ho Chi Minh , pia kimeathirika sana.

Maafisa wamewaondoa mamia kwa maelfu ya wakaazi wa eneo hilo kabla ya kimbunga hicho kushambulia.

Alhamis wiki iliyopita zaidi ya watu 1,000 wamehofiwa kufa nchini Philippines katika maporomoko makubwa ya matope yaliyosababishwa na mvua kutokana na kimbunga hicho Durian.