1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hofu ya mashambulizi ya al-Qaeda yatanda

6 Agosti 2013

Mada zilizowashughulisha zaidi wahariri wa magazeti hii leo(06.08.2013) ni pamoja na tahadhari iliyotolewa na Marekani kuhusu mashambulizi ya kigaidi dhidi ya balozi zake, tuhuma za "doping" wanamichezo.

https://p.dw.com/p/19KQo
ARCHIV - Polizisten stehen auf der Tower Bridge in London (Archivfoto vom 03.06.2012). Knapp drei Wochen vor Beginn der Olympischen Spiele in London hat die Polizei sechs Terrorverdächtige festgenommen. Es bestehe der Verdacht der Anstiftung, Vorbereitung und Beauftragung von Terrorakten, teilte die Polizei am Donnerstag mit. Eine direkte Verbindung zu den Olympischen Spielen gebe es nicht. Die Polizei hatte am frühen Morgen eine Wohnung in London gestürmt. EPA/TAL COHEN +++(c) dpa - Bildfunk+++
Tahadhari ya shambulio la kigaidi nchini Uingereza polisi wakishika doriaPicha: picture alliance / dpa

Miaka miwili iliyopita ilionekana kuwa kundi la al-Qaeda limeshindwa. Vijana wa Kiarabu walizinduka kwa amani , bila ya kutumia nguvu na waliwaondoa madarakani watawala wa kimabavu.

Nadharia ya kundi la al-Qaeda ya kutumia nguvu kuanzisha taifa la Kiislamu na kupambana ili kutumia hukumu za sharia kama njia pekee ya sheria za nchi, Ikiwa ni Bin Laden ama mrithi wake Zawahiri, vijana wa mataifa ya Kiarabu hawawasilikizi tena watu hao wenye mawazo ya kizamani, ambao wamekuwa wakijificha katika maeneo ya Hindukush.

Vijana hawa wanapendelea kufuata badala yake mapinduzi yao yaliyowafikisha hapa. Lakini al-Qaeda imerejea na imeanza kuleta hofu kupitia ugaidi. Mhariri anasisitiza kuwa kundi la kizazi kipya cha al-Qaeda limejifunza mengi kutokana na kudhoofika na pia makosa iliyoyafanya.

Nalo gazeti la Hannoversche Allgemeine likiandika kuhusu tahadhari hiyo ya ugaidi linasema.

Kutokana na kuongezeka tena kwa hatari ya ugaidi, hakuna suluhisho rahisi kwa sasa. Mataifa ya magharibi yanapaswa kuikubali hali hiyo, kwamba kitisho hicho kitakuwapo kwa muda mrefu ujao na ni kwa njia ya kijeshi tu yanaweza kujaribu kuizuwia hali hiyo lakini sio kuondoa kabisa.

Polizisten kontrollieren am Mittwoch (17.11.10) auf dem Flughafen in Hamburg einen Reisenden. Die Lufthansa rechnet nach der Terror-Warnung von Innenminister Thomas de Maiziere (CDU) nun mit verschaerften Sicherheitskontrollen auf den Flughaefen. Das sagte Firmensprecher Thomas Jachnow am Mittwoch in Frankfurt am Main. Dafuer sei die Bundespolizei zustaendig. "Terroristen muessen am Boden unschaedlich gemacht werden", sagte er. (zu dapd-Text) Foto: Axel Heimken/dapd
Polisi wa Ujerumani wakipekua watuPicha: dapd

Gazeti la Badische Zeitung linalochapishwa mjini Freiburg lina maoni kuwa kitisho hiki cha ugaidi kutoka kwa al-Qaeda kitazidisha uhalali wa kuchunguzwa mawasiliano ya simu na mtandao na kwamba bila kufanya hivyo itakuwa hatuna uwezo wa kuzuwia ama kutambua nini kitafanyika. Mhariri anaongeza kusema.

Hivi sasa tunafahamu mipango hiyo ya kigaidi na tunaweza kuishinda. Lakini pamoja na hayo kundi hilo la kigaidi hivi sasa linapanga kitu kingine. Nani analipinga hilo ? Mzizi wa jambo hili hapa hata hivyo ni kwamba mbinu hizi haziwezi kuthibitishwa kuwa ni sasa na hatujui pia matokeo yake.

"Doping"

Ujerumani magharibi pamoja na mataifa mwengine ya magharibi yalikuwa kimya kwa muda mrefu katika enzi zile za vita baridi kuhusu masuala ya matumizi ya madawa ya kuimarisha misuli katika michezo , yaani "doping". Mataifa ya magharibi yalitaka kujionesha kuwa ni bora kuliko yale ya mashariki katika michezo. Kwa hali hii yalijipatia medali nyingi na kujiweka katika hali kwamba mataifa hayo yamejitenga na uchafu wa udanganyifu katika michezo. Hali hiyo sasa haiko tena kama anavyosema mhariri wa gazeti la Thüringische Landeszeitung.

Watu kama mashine kutoka mataifa ya mashariki dhidi ya wanamichezo wanaofanya michezo kwa ridhaa yao kutoka mataifa ya magharibi, ambao ni bora , kwasababu wana mfumo sahihi wa uongozi. Hatimaye tumeanza kujiuliza kuhusu usafi wa mamlaka zinazohusika , ambazo zimekuwa zikiwapa wanamichezo dawa hizo za kutunisha misuli. Maafisa hawataweza tena kuziba taarifa hizi kujitokeza hadharani. Na mhariri anasisitiza kuwa uwazi ni kitu muhimu.

Ein Röhrchen mit Kunstblut wird am 09.01.2013 in einer Stallung in Riesenbeck (Nordrhein-Westfalen) im Rahmen einer gestellten Dopingkontrolle gezeigt. Die Nationale Anti-Doping-Agentur (NADA) gibt einen Blick hinter die Kulissen einer Pferdekontrolle. Foto: Friso Gentsch dpa
Udhibiti wa matumizi ya dawa za kuongeza nguvu misuliPicha: picture-alliance/dpa

Siku ya kula mboga

Mada kuhusu siku ya kutokula nyama na kuongeza matumizi zaidi ya mboga mboga. Mhariri wa gazeti la Mannheimer Morgen anaandika.

Kwa uamuzi , iwapo mtu apendelee kula nyama ama mboga mboga , hili ni jambo ambalo linahitaji uhuru wa kuamua. Yule anayetaka kujipatia afya , hahitaji nadharia za ushauri, badala yake anahitaji mtu huyu mtazamo wenye uwiano. Kwa kutumia mantiki tu , mtu anapaswa kufanya uchaguzi sahihi na kujipatia nyama yenye ubora wa hali ya juu lakini atalipa fedha nyingi. Katika wakati huu wa majira ya joto hapa barani Ulaya siku kama hii ya kula mboga mboga tu ni jaribio linaloelekea kisiasa kutafuta kura kabla ya uchaguzi wa hapo Septemba nchini Ujerumani. Mhariri anasisitiza kuwa chama cha Kijani kinaonekana hapa kuwa kinatumia mbinu za mwalimu mkuu wa shule na sera zake haziwahusishi zaidi wazee wa taifa hili.

Mwandishi : Sekione Kitojo / inlandspresse

Mhariri : Mohammed Abdul-Rahman