1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Holland na Urusi leo

20 Juni 2008

Kombe la Ulya linaendelea leo kwa Holland ikania tiketi ya nusu-finali kutoka Russia.

https://p.dw.com/p/ENay
Van Basten ana miadi na Guus Hiddink leo.Picha: pa / dpa

Baada Croatia na Uturuki jana usiku kunyan'ganyia tiketi ya pili ya nusu-finali ya kombe la Ulaya la mataifa, leo ni changamoto kati ya makocha 2 wa kidachi:Marco van Basten anaeiongoza Holland na Guus Hiddink -Urusi.Kiasi cha mashabiki 50.000 wa Uholanzi watazamiwa leo kumiminika mjini Bern na kuupaka mji huo wa Uswisi, rangi ya manjano.Tangu jana mashabiki hao wakijikusanya mjini Basel kwa mechi ya leo na Urusi.

Kesho jumapili itakua zamu ya mabingwa wa dunia-Itali kupapurana na jirani zao Spain.

►◄

Stadi wa Russia,Andrei Arshavin amemuonya kocha wa Holland, Marco van Basten kutarajia hujuma kali za washambulizi wao kuzidi kasi leo hii Russia inapokumbana na Holland kuania tiketi ya nusu-finali alhamis ijayo.

Arshavin hakuweza kucheza mechi 2 za kwanza za Russia kwavile, alifungiwa kucheza,lakini aliporudi uwanjani juzi wasweden walipata habari zake.Alitoa pasi kwa Roman Pavvlycchenko kutia bao lwa kwanza la russia katika lango la Sweden na mnamo dakika ya 50 ya mchezo akaufamania binafsi malngo wa sweden kwa bao la pili la Russia.

Hizo ndizo salamu Arshavin alizotoa kwa kocha van basten. Jogoo huyu wa klabu ya St.Petersberg,anawika kweli na ikiwa Holland haikuchunga leo, basi itakua Russia chini ya kocha mdachi guus Hiddink ikitoroka na tiketi ya nusu-finali kwa miadi alhamisi ijayo ama na Itali au na Spian.

Mpambano wa leo kati ya Russia na Holland ni wa pekee kwa Guus Hiddink,kocha wa russia mwenye umri wa miaka 61 na alieiongoza Holland hadi nusu-finali ya Kombe la dunia,1998 nchini Ufaransa na kutolewa na Brazil katika changamoto za mikwaju ya penalty.

Holland lakini ndio ilikosha nyoyo za mashabiki wengi wa sdimba katika kombe hili la Ulaya:

Kwanza waliwashikisha adabu mabingwa wa dunia Itali kwa kuwakomea mabao 3:0.halafu ikawa zamu ya makamo bingwa wa dunia-Ufaransa kuchezeshwa kindumbwe-ndumbwe na kufungishwa virago kwa mabao 4:1.

Sasa,Holland itairuhusu Russia kuitilia kitumbua chake mchanga jioni hii ?

Kocha van basten anaejiuzulu baada ya kombe hili la Ulaya ili kuwa kocha wa klabu yake ya zamani Ajax Amsterdam, amesema duru ya kwanza ilifurahisha,lakini kazi inaanza sasa katika duru hii ya kutoana.

Wadachi watawategemea tena akina van Niestelrooy,van der Vaart,van Persie na van der saar,kutamba tena leo na kuepuka wembe uliowanyoa wafaransa na wareno hauwanyoi wao.

Kesho jumapili itakua asie na mwana aeleke jiwe na asie na mguu atie gongo-mkutano mjini Vienna,Austria:

Mabingwa wa dunia-Itali waliowapiga kumbo wafaransa majuzi wana miadi na jirani zao Spian. Spian inafahamika kupepesuka pale inapohitaji kutamba na wengi wanaitarajia kukumbwa na hatima hiyo hiyo kesho mbele ya Itali,licha ya kuwa waspain wameshinda mechi zao 3 zote zilizopita kinyume na Itali.

Miaka 2 iliopita, Spian ilishinda mechi zake zote 3 za kundi lake katika kombe la dunia hapa Ujerumani.Mwishoe, lakini ikatolewa na Ufaransa katika duru ya pili ya kombe la dunia.

Kinachokatisha tamaa zaidi ni historia yao na Itali: Katika miaka 88 iliopita na mapambano 3 yaliopita kati ya timu hizi mbili, Spian haikuwahi kuwika mbele ya mabingwa wa dunia Itali.Waazuri watatunisha misuli kesho kuseleleza mila hiyo.Waspian watataka kuvunja mwiko .