1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Homa ya dimba imepiga Khartoum leo

18 Novemba 2009

Algeria na Misri-nani ataondoka na tiketi ya kombe la dunia ?

https://p.dw.com/p/Ka8j
Dimba Afr.kusini 2010

Macho ya mashabiki wa dimba barani Afrika na nje yake, yanakodolewa wakati huu Khartoum,Sudan ambako jioni hii, mabingwa wa Afrika ,Misri na mahasimu wao wa jadi Algeria,wanaingia uwanjani Oumduraman,upande wapili wa Khartoum, kuania tiketi ya mwisho kanda ya Afrika kwa Kombe lijalo la dunia nchini Afrika kusini.Nani atashinda ,na vipi kuzima jazba na fujo la walioshindwa,ni mtihani wa polisi na vikosi vya ulinzi tangu mjini Khartoum,Cairo na hata Algeirs,kwani, hii, ni finali ya kwanza ya Kombe la dunia 2010 barani Afrika:

Yafaa hata kusema kwamba, "huu ni mpambano wa kufa-kupona" kwa mataifa haya 2 ya dimba ya Afrika kaskazini. Gavana wa Khartoum, Abdelrahman al-Khid, amearifu jana kuwa, anatazamia safari za ndege 48 kutoka Algeria na 18 kutoka jirani Misri.

Mji wa Khartoum, umegeuzwa "Mecca ya dimba" na haukuwahi maishani mwake, kujionea umati wa mahujaji ambao wamegeuza dira badala ya kwenda Mecca,Saudia Arabia, wanawasili Khartoum kwa finali hii ya kwanza ya Kombe la dunia. Ukumbi wa abiria wa Uwanja wa ndege mjini Khartoum,ni bahari ya bendera na jazi za kijani na nyeupe za mashabiki.

Shabiki mmoja wa Algeria amenukuliwa kusema, "Nimewaacha n yumbani mke wangu na wanangu 2.Nimeacha kila kitu ili kuja hapa."-alisema Abdel.

Taarifa zinasema kuna mashabiki waliowasili Khartoum wakiwa hana chochote mfukoni,mradi tu waawe karibu na timu yao.Misri imehanikiza kuilalamikia Algeria kwa fujo inayofanyiwa na mashabiki wa Algeria baada ya basi la wachezaji wa algeria kushambuliwa kwa mawe mjini Cairo ijumaa iliopita.

Waziri wa nje wa Misri Ahmed Abul Gheit, amesema amemtaka waziri mwenzake wa mambo ya nje wa Algeria, Mourad Medelci, kuwa serikali yake ipambane na wafanya fujo .Kwani, shirika la simu za mkono la misri ORASCOM Telecom limetangaza linawahamisha watumishi wake 25 na familia zao kutoka Algeirs baada ya afisi zake 15 nchini Algeria kuharibiwa.Hata afisi za Egypt Air-shirika la ndege la Misri,zimehujumiwa tena mara kwa mara.

Algeria na Misri, ni timu 2 zenye historia ndefu ya uhasama mkubwa wa dimba.Kwani, machafuko yalizuka pale Misri ilipoilaza Algeria kwa bao 1:0 1989, mjini Cairo na kuipiga kumbo nje ya kombe la dunia,1990 nchini Itali .

Chama-tawala nchini Misri, "National Democratic Party" cha rais Hosni Mubarak,kimetoa sadaka kwa mashabiki 2000 tiketi za bure kwenda Khartoum kuwashangiria mafiraouni.Kwani, kombe la dunia barani Afrika, bila mabingwa wa Afrika-Misri haiwezekani.

Na sio tu mashabiki wa Misri hao wamepewa tiketi za bure, bali pia usafiri na malazi bure hotelini .Hoteli zote mjini Khartoum, hazina tena nafasi tangu jana.Sudan , imetayarisha kambi tofauti kwa mashabiki wa Algeria na wa Misri, na FIFA imeamrisha si zaidi ya mashabiki 35.000 waruhusiwe uwanjani Oumduraman,uwanja unaochukua mashabiki 41.000.Lengo ni kuwatenganisha mashabiki wa timu hizo mbili.

Sitapenda kuagua vipi mpambano huu utamalizika tangu uwanjani hata mitaani na sio tu huko Afrika kaskazini bali hata Marseille,Ufaransa.