1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Homa ya kujua Papa anatokea wapi

12 Machi 2013

Zoezi la kumchagua kiongozi mpya wa kanisa katoliki ulimwenguni,ajali ya moto huko Backnang,mbinu za waziri mkuu wa Hungary na SPD na kivuli cha ajenda 2010 magazetini

https://p.dw.com/p/17vPi
Makadinalai wanafuatilizia misa ya kabla ya zoezi la kumchagua Papa mpyaPicha: picture-alliance/dpa

Tuanzie lakini Vatikan ambako hii leo makadinali 115 wanatarajiwa kuanza zoezi la kumchagua kiongozi mpya wa kanisa katoliki.Gazeti la "Hannoversche Allgemeine" linaorodhesha masuala anayoweza kuyashughulikia kiongozi mpya wa kanisa katoliki ulimwenguni.Gazeti linaandika:

Papa mpya anaweza kwa mfano kubatilisha haraka au angalao kuregeza makali ya hali ya Utawa.Hata katika mkabala wa wajane walioamua kuowa au kuolewa tena ambao kwasasa wanatengwa katika sakramenti,kuna upenu wa marekebisho.Lakini wapenda mageuzi wasifurahie mapema:Kanisa halitoanza upya kujaa kwasababu ya mageuzi.Katika kanisa la kiinjili  marekebisho yametekelezwa lakini hata hivyo idadi ya waumini wanaolipa kisogo ni kubwa kulike ile ya kanisa katoliki.Benedikt wa 16 hakukosea aliposema "tatizo halikutikani pekee katika mzozo kanisani,bali katika mzozo wa imani.

Wahariri wa magazeti ya Ujerumani wamejishughulisha pia na mbinu za waziri mkuu wa Hungary za kuifanyia marekebisho katiba kwa lengo la kung'ang'ania madaraka.Gazeti la "Lausitzer Rundschau" linaandika:

La kusikitisha zaidi ni ile hali kwamba kundi la wahafidhina katika bunge la Ulaya wakiwemo pia wana CDU/CSU,daima limekuwa likiwaepushia lawama washirika wao wa chama cha Fidesz kinachoongozwa na Viktor Orban.Upande wa upinzani mjini Budapest umekasirishwa na kuzungumzia kuhusu "Aibu ya Ulaya."Msimu wa kiangazi mwakani,Orban anataka achaguliwe tena.Anaweza kuchochea mambo kupitia mageuzi ya utaratibu wa kupiga kura au sera zake kuelekea vyombo vya habari.Lakini kughoshi matokeo ya uchaguzi hatoweza.Kwa hivyo upande wa upinzani hauna nafasi kubwa ya kuweza kumzuwia Orban asisonge mbele.

Janga la moto laangamiza watu wanane

Backnang Brand Gedenken Blumen und Kerzen
Mashada ya mauwa na mishumaa kuwakumbuka wahanga wa ajali ya moto huko BacknangPicha: picture-alliance/dpa

Ajali ya moto iliyoangamiza maisha ya watu wanane.wote wa kutoka familia moja huko Backnang imewahuzunisha wengi nchini Ujerumani.Gazeti la "Stuttgarter Nachrichten" linaandika.

Watu wanane wamepoteza maisha yao katika ajali hiyo ya moto.Binaadam.Sio watu wa taifa fulani.Ukweli kwamba wahanga hao wanane,wakiwemo watoto sabaa,wana uraia wa Uturuki,haubadilishi chochote katika msiba huo.Hata hivyo uraia unachangia kwa njia moja au nyengine katika kutathmini ajali hiyo.Jibu rasmi kutoka Uturuki linaashiria ukosefu wa hali ya kuaminiana.Kuna mengi yaliyowahi kutokea.Au kama wataalam wa Uturuki wanavyosema:"Kuna suala la kuulizwa linalowekwa baada ya tukio kama hili la Backnang."

Ajenda 2010

xel
Mwenyekiti wa chama cha SPD Sigmar Gabriel (kulia)na mgombea wa kiti cha rais Peer Steinbrück wakitangaza mpango wa chama chaoPicha: picture-alliance/dpa

Na mada yetu ya mwisho inahusiana na chama cha upinzani cha Social Democratic na juhudi zake za kuwavutia wapiga kura.Gazeti la "Neue Presse" linaandika:

Kulingana na utafiti wa maoni ya umma,chama cha SPD kiko nyuma ya CDU na mgombea wake ndo kabisa,anaburura mkia nyuma ya Angela Merkel.Hata hivyo SPD hawana sababu yoyote ya kutaharuki.Katika mipango yao kuelekea uchaguzi mkuu,wanatanguliza mbele masuala ya jamii ambayo yanaonyesha kuwavutia wapiga kura.Na pindi Peer Steinbrück akifanikiwa kutoteleza mara kwa mara,anaweza kuwafanya wapiga kura wathamini anachokipigania.Pengo linalomtenganisha na Angela Merkel hadi september linaweza kupungua.

Mwadishi :Hamidou Oummilkheir/Inlandspresse

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman