1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Homa ya nguruwe

Oumilkher Hamidou27 Aprili 2009

Juhudi za kuzuwia homa ya nguruwe isitapakae ulimwenguni

https://p.dw.com/p/Hf52
Nguruwe katika shamba moja nchini MexicoPicha: AP


Mada kuu magazetini hii leo ni kuhusu homa ya nguruwe na kura ya maoni ya Berlin kuhusu mafunzo ya dini shuleni.

Tuanze na gazeti la LEIPZIGER VOLKSZEITUNG linaloandika kuhusu homa ya nguruwe.Gazeti linaendelea kuandika:

"Hofu zimeenea tena.Watu walikua wameshazisahau picha za mabata waliokufa na kuku waliokua wakishikiliwa kwa nguvu ndani ya mabanda.Kwa mujibu wa wataalam wa shirika la afya la kimataifa,WHO, jinamizi la homa ya nguruwe linatajikana kua hatari zaidi kupita lile la homa ya ndege.Kwasababau safari hii jinamizi hili linatishia kugeuka maradhi hatari ya kuambukiza.Hofu hizo si za bure hata kama zimeripuka katika nchi yenye uwezo wa kuzituliza.Hata kama rais wa Mexico Calderon ametia njiani hatua kali za kukabiliana na kitisho hicho,hata hivyo ripoti kutoka maduka ya madawa,ambako zana watu wanazofunga kuanzia pua hadi mdomo, kujikinga dhidi ya maradhi ya kuambukiza zimekwisha ,zinamfanya mtu ashuku kama juhudi za serikali za kukabiliana na kishindo hicho zinatosha.

Gazeti la MÄRKISCHE ODERZEITUNG linaandika:

"Shirika la afya la kimataifa WHO linahofia,aina hii mpya ,inaweza kusababisha maradhi ya kuambukiza.Watu wanabidi wawe na tahadhari.Wataalamu wamekua kwa muda mrefu sasa wakionya dhidi ya kuzuka maradhi hatari ya kuambukiza kote ulimwenguni.La muhimu katika hali kama hiyo ni kuchukua haraka hatua zinazohitajika.Katika kishindo cha homa ya mafua ya ndege,China ilipitisha muda mrefu hadi ilipoamua kuchapisha maelezo kuhusu maradhi hayo.Mexico haijapoteza wakati,imetangaza hapo hapo,ili kuyapatia nafasi mataifa mengine ya kuchukua hatua za kinga.

Sasa tunaelekea Berlin.Gazeti la FRANKFURTER RUNDSCHAU linaandika kuhusu matokeo ya kura ya maoni kuhusu masomo ya dhini shuleni.Gazeti linaendelea kuandika:

Imeshapita.Si haba.Wakaazi wa Berlin wameamua na wameamua ndivyo hasa.Baada ya kampeni kali ya miezi kadhaa iliyoendeshwa na makanisa,utaratibu wa shule utaendelea kua kama zamani mjini Berlin.Angalao linapohusika suala la dini:Waislam,wayahudi ,wakristo,mabudha na wengineo wasioamini dini wataendelea kwa pamoja kutafakari darasani juu ya umuhimu wa maadili katika jamii.Masomo hayo ni pamoja na mfumo wa imani na kufikiria njia ya maana ya kuwajibika katika jamii.Anaetaka kuchagua mafunzo ya dini anaweza.Hakuna shida".

Muandishi:Hamidou Oummilkheir


Mhariri Abdul Rahman