1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HONIARA:Waathirika wa tsunami katika visiwa vya Solomon waanza kusaidiwa

3 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCCt

Misaada ya dharura imeanza kuwasili katika visiwa vya Solomon vilivyokumbwa na tufani ya tsunami.

Boti iliyobeba vyakula na mahitaji mengine ya dharura iliwasili huko magharibi mwa jimbo la Gizo.

Kiasi cha watu 20 waliuawa na mamia kadhaa hawana makazi baada ya tsunami kuvikumba visiwa hivyo hapo jana.