1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hotuba ya kansela Merkel bungeni mjini Berlin

P-Stützle / Oummilkheir24 Mei 2007

Kansela aachambua malengo ya mkutano wa kilele wa G8 mjini Heiligendamm

https://p.dw.com/p/CHDp
Picha: AP

Mkutano wa kilele wa viongozi wa mataifa manane tajiri kwa viwanda-G8, utakaofanyika kuanzia June sita had inane ijayo mjini Heiligendamm,ndio mada iliyoingia midomoni kwa sasa nchini Ujerumani.Kinachojadiliwa zaidi lakini ni kuhusu hatua za usalama na maandamano yanayopangwa kuitishwa dhidi ya mkutano huo wa kilele utakaowaleta pamoja viongozi wa mataifa tajiri kwa viwanda na Urusi.Hii leo,kansela Angela Merkel,ambae ndie mwenyekiti wa sasa wa G8-amechambua sera za jumuia hiyo bungeni pamaoja na kuelezea malengo waliyojiwekea.

Utandawazi sio tuu katika nchi zao,bali kote ulimwenguni-hilo ndilo lengo la G8-amesema kansela Angela Merkel katika taarifa yake bungeni hii leo mjini Berlin.“Ukuaji wa kiuchumi na kuwajibika” ndio kauli mbiu ya mkutano wa kilele wa viongozi wa mataifa tajiri kwa viwanda mjini Heiligendamm.Na kauli mbiu hiyo inamaanisha kwamba mataifa manane tajiri kwa viwanda yanabidi yawajibike kikamilifu katika masuala ya maendeleo-amesisitiza kansela Angela Merkel.

Lakini maendeleo hayawezekani bila ya kujumuishwa pia mataifa yanayoinukia mfano China,India na Brazil-ndio maana viongozi wan chi hizo wamealikwa kuhudhuria mkutano wa kilele wa Heiligendamm.

Malengo sabaa muhimu ameyataja kansela Angela Merkel kwaajili ya mkutano huo wa kilele-na maendeleo kwa bara la Afrika ndio kipa umbele anasisitiza kansela Merkel:

“Kwa upande mmoja,ahadi dhabiti tulizotoa katika kipindi cha miaka iliyopita ili kuongeza misaada ya maendeleo itaanza kuleta tija.Nnasema wazi wazi tutaheshimu ahadi hizo.Lakini tunataka pia washirika wetu wa Afrika waendelee kwa bidii zaidi kutia njiani mageuzi.“

Kansela Angela Merkel amependekeza pia faida zitakazotokana na kuuzwa vyeti vya kupunguza moshi wa viwandani,utaratibu uliotajwa katika juhudi za kuhifadhi hali ya hewa-faida hizo zitumiwe pia kugharimia miradi ya maendeleo.

Hifadhi ya hali ya hewa ni mojawapo ya malengo sabaa katika mkutano wa kilele wa Heiligendamm-yakizingatiwa masilahi ya jamii katika utaratibu jumla wa utandawazi-njia bora za kulinda mifuko ya hazina ya kinga ambayo kansela Angela Merkel anasema inatoa kitisho kwa uchumi wa dunia pamoja na utaratibu wa biashara huru ya dunia.

Ingawa katika hotuba yake bungeni kansela hakufafanua kwa undani kabisa yaliyomo ndani ya malengo hayo sabaa hata hivyo kansela Angela Merkel amesisitiza serikali ya shirikisho inatilia maanani wasi wasi wa wakosoaji wa mfumo wa sasa wa kiuchumi ulimwenguni.Kansela Angela Merkel ameendelea kusema:

„Anaetaka kutumia nguvu,ajue hapo anaondowa uwezekano wa kujadiliana.Nnasema wazi kabisa:wale wenye kukosoa hii leo hatua za usalama,ndio wale wale watakaokua wa mwanzo kupaza sauti kuwakosoa maafisa wa usalama pindi machafuko yakitokea.Kinyume chake lakini ni kwamba,na hapa nnasema wazi wazi pia,atakaetaka kuandamana kwa amani,madai yake sio tu uni ya haki,bali tutayazingatia pia.“

Upande wa upinzani wa FDP,walinzi wa mazingira na Die Linke wametilia shaka kama malengo hayo yatafikiwa viongozi wa mataifa tajiri kwa viwanda watakapokutana mjini Heiligendamm.