1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hotuba ya Rais Bush kwa Taifa

14 Septemba 2007

Rais George Bush wa Marekani ametangaza kwa mara ya kwanza kurejesha nyumbani sehemu ya majeshi ya Marekani yaliopo Irak.Upinzani chama cha Democrat hakijaridhika na tangazo lake.

https://p.dw.com/p/CB1F
George Bush
George BushPicha: AP

Rais George Bush wa Marekani, alilihutubia taifa jana usiku kwa njia ya TV kuchambua upya sera zake juu ya Irak.Tayari mwanzoni mwa wiki hii,amirijeshi mkuu wa Marekani nchini Irak,jamadari David Petraeus na balozi wa Marekani nchini Irak,Ryan Crocker,waliripoti juu ya hali ya mambo ilivyo nchini Irak.

Rais george Bush aliitikia mapendkezo ya amirijeshi wake mkuu nchini Irak,jamadari Prtraeus.Hadi siku kuu za x-masi mwaka huu,atawarejesha nyumbani askari 5.700.

Akitaja juu ya mafanikio ya kijeshi iliopata Marekani nchini Irak,Bush aligusia hali ya usalama iliotengenea katika mkoa wa Anbar na Diyala pamoja na katika mji mkuu Baghdad.

Kutengenea huko kwa hali ya uslama ,alisema Bush kutawezesha hata hapo Julai,mwakani kubakisha nchini Irak vikosi 15 kati ya vote 20 vya Marekani viliopo nchini Irak.

Hii itafanya idadi ya askari wa Marekani watakaobaki Irak kuwa sawa kama ilivyokuwa kabla rais Bush hakuanza kuongeza idadi ya vikosi hivyo, Januari mwaka huu.

Mwezi Machi mwakani,jamadari Petraeus atapaswa kutoa ripoti mpya ya makisio juu ya hali nchini Irak.Bush katika hotuba yake jana usiku akasema:

“Msingi ninaoegemeza uamuzi wangu juu ya idadi ya wanajeshi nchini Irak, ni ule wa “ kurejesha vikosi kulingana na mafanikio”.

Kila tukifanikiwa zaidi,ndipo askari zaidi waweza kurejea nyumbani.Lakini katika kila tufanyacho, nitahakikisha amirijeshi mkuu huko Irak, ana mamlaka na askari wa kutosha ili kumshinda adui.”

Bush lakini, hakutaja ni chini ya misingi gani anapimia mafanikio aliotaja.Lakini, kwa mara ya kwanza jana amezungumzia kuwarejesha baadhi ya wanajeshi nyumbani kutoka Irak na hapo ameanza kuitikia madai ya wapinuzani wake wa vita vya Irak.Anatumai Bush kuziba mwanya wa tofauti kati yake na wapinzani wake wa chama cha Democrat.

“ Njia niliosimulia ,infanya kwa mara ya kwanza iwezekane,kuwaleta pamoja watu ambao wamekuwa na msimamo tofauti katika mjadala huu .”

Wafuasi wa chama cha Upinzani cha Democratic Party,lakini walikwishabainisha wazi hawaoni lolote jipya katika tangazo la jana la rais Bush.Ikiwa jibu rasmi la wademocrat kwa hotuba ya George Bush,seneta Jack Reed wa Rhode Island alisema,

“Kwa mara nyengine tena rais amekosa kutoa mpango wenye madhubuti kuonesha jinsi gani anapanga kuvikomesha vita.Wala hakutoa hoja yenye nguvu kuviendeleza vita hivyo.”

Alisema seneta Reed. Wademokrat halkadhalika, watajaribu kwa njia nyengine zaidi kubadili jukumu la wanajeshi wa Marekani nchini Irak kwa jinsi watakavyo wao.Hadi sasa wameshindwa kutokana na kutoungwa mkono vyakutosha na wabunge wa chama-tawala cha Republican katika Congress-Bunge la Marekani.

Bush alisema pia katika hotuba yake kwamba ameiwekea wazi serikali ya Irak ya Al Maliki,inapaswa kuleta utulivu wa kisiasa nchini.

Bush aliwasangaza wengi alipotaja kwamba majeshi ya Marekani kwa kadiri Fulani yatabakia Irak hata baada ya kipindi chake cha wadhifa wa urais kinachomalizika baada ya uchaguzi wa mwakani.