1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Huduma ya Intaneti yazimwa Senegal

13 Februari 2024

Huduma ya mawasiliano ya intaneti imezimwa nchini Senegal saa chache baada ya mamlaka za nchi hiyo kuzuia maandamano yaliyopangwa kufanyika mapema Jumanne kupinga kusogezwa mbele uchaguzi uliopangwa kufanyika mwezi huu.

https://p.dw.com/p/4cM3o
Maandamano katika mji wa Dakar, Senegal
Waandamanaji DakarPicha: Zohra Bensemra/REUTERS

Wizara ya mawasiliano ya nchi hiyo imetangaza kuwa huduma ya intaneti inasitishwa kwa sababu mitandao ya kijamii inatumika kusambaza ujumbe wa chuki ambao tayari umechochea maandamano ya vurugu.

Kwa siku kadhaa sasa Senegal imekumbwa na wimbi la maandamano yaliyochochewa na uamuzi wa Rais Macky Sall la kuuahirisha uchaguzi wa rais uliopangwa Februari 25, katika wakati uongozi wake mihula miwili unaelekea kufikia mwisho.

Umoja wa Mataifa umesema hii leo kwamba unatiwa wasiwasi na mivutano inayoshuhudiwa nchini humo na kuitolea mwito serikali ya Sall kuulinda utamaduni wa miongo mingi wa Senegal wa kuheshimu demokrasia na haki za binadamu.