1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Athari za mapigano kwa wakaazi wa Goma

5 Februari 2024

Jiji la Goma lenye idadi ya watu zaidi ya milioni 2, linategemea kikamilifu chakula kutoka kwa nchi jirani za Rwanda, Tanzania, Uganda na Kenya, kufuatia vita kati ya jeshi la Kongo na waasi wa M23.

https://p.dw.com/p/4c4d6
Afrika Kongo Goma
Sehemu ya mji wa Goma, Jamhuri ya Kidemokrasia ya KongoPicha: Ben Curtis/AP/picture alliance

Jiji la Goma lenye idadi ya watu zaidi ya milioni 2, linategemea kikamilifu chakula kutoka kwa nchi jirani za Rwanda, Tanzania, Uganda na Kenya, kufuatia  vita kati ya jeshi la Kongo na waasi wa M23

Mji mdogo wa Sake na jiji la Goma imekosa usambazaji wa bidhaa za chakula kutoka Minova na Bweremana. Hali hii inalazimisha jiji la Goma kutegemea zaidi usafiri wa majini, ambayo ni wa kienyeji. Tuliwauliza madereva wa malori ya usambazaji kutoka Shasha. Amani Elia ni mmoja wao.

M23
Waasi wa M23 wakijiondoa mji wa MasisiPicha: Jerome Delay/AP/picture alliance

"Hali ni mbaya kwa sababu ya milio ya risasi. Barabara bado haijafungwa, waasi wako karibu na barabara. Wakati mwingine mtu anaweza kutumia kusafirisha chakula lakini kuna hofu njiani. Sasa hatuna chakula. Tunaiomba serikali yetu imalize vita."

Watu wa Goma wanaelezea wasiwasi wao kuhusu mgogoro huu. Wanahofia upungufu wa chakula unaoweza kutokea. 

Uhusiano kati ya Rwanda na Burundi unayumba zaidiZaidi ya hayo, sasa jiji linategemea uagizaji wa chakula kutoka Rwanda, Tanzania, Kenya na Uganda kupitia mpaka mdogo wa Goma. Hata hivyo, harakati za watu zimezuiliwa kwenye mpaka kati ya DRC na Rwanda, kutokana na uamuzi wa Kinshasa dhidi ya uvamizi wa Rwanda.

Kongo -Goma
Wakaazi wa GomaPicha: Arlette Bashizi/REUTERS

Je, kupungua kwa harakati kwenye mpaka kutakuwa na athari za moja kwa moja kwenye usambazaji wa vyakula? Pepe Mikwa, msimamizi wa mawasiliano wa mradi wa kurahisisha biashara ya mpakani, anaeleza, " Inaomba kueleweka kwamba chakula tunachokula Goma kupitia mpakani hutoka si tu Rwanda, bali pia Uganda, Tanzania, Kenya, Burundi, n.k. Hivyo, Masisi na Rutshuru zikikumbwa na vita, naamini chakula kutoka nchi nilizotaja kitazidi kuingia mjini."

Soma: Takriban raia 20 wauawa kwenye shambulizi nchini jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo

Huku waasi wa M23 wakiongeza nguvu zao na kuendelea kuchukua ardhi jimboni kivu kaskazini na kusonga mbele polepole kuelekea kivu kusini, Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Felix Tshisekedi anabaki imara kwa kukataa kabisa kujadili na waasi hao hata kama hali itakuwaje.