1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hukumu ya kifo yafutwa katika jimbo la New Jersey- Marekani

14 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CbgP

Jimbo la Marekani la New Jersey,limekuwa la kwanza nchini humo, katika kipindi cha miongo minne, kupiga kura kuondoa hukumu ya kifo. Hatua hiyo imesifiwa na makundi yanayotetea haki za binadamu yakisema ni hatua moja kuelekea kukomesha hukumu hiyo kali.Bunge la jimbo hilo ambalo linadhibitiwa na wademokrati, limebadilisha hukumu ya kifo na kuifanya kifungo cha maisha.