1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hukumu ya Mubarak kutolewa

31 Mei 2012

Rais wa Misri aliyetolewa madarakani mapema mwaka jana Hosn Mubarak, wanawe wakiume wawili na maofisa kadhaa wa usalama wanatarajiwa kujua hatima yao mahakamani Juni 2 mwaka huu.

https://p.dw.com/p/155xk
Alaa na Gamal Mubarak wakiwa mahakamani Cairo , Nchini Misri
Alaa na Gamal Mubarak wakiwa mahakamani Cairo , Nchini MisriPicha: AP

Katika hukumu juu ya tuhuma kadhaa zinazowakabili zikiwamo za rushwa na mauaji ya waandamanaji .

Kiongozi huyo, wanawe wawili wakiume na makamanda wa vyombo vya usalama wanatumiwa kwa makosa ya mauaji ya waandamanaji 850 ambao walifariki katika siku18 za mapinduzi yalioung'oa utawala wa kiongozi huyo uliodumu kwa miongo mitatu.

Katika tuhuma za rushwa zinazomkabili Mubarak , ni kuuzwa kwa benki ya Al-Watany ambapo yeye na familia yake walinunua hisa zote ambazo zlipaswaa kununuliwa na watu wa kawaida. Sambamba na hilo walichota Euro milioni 300 na kuzificha katika mabenki za ng'ambo.

Aliyekuwa Rais wa Misri Hosn Mubarak akiwa mahakamani
Aliyekuwa Rais wa Misri Hosn Mubarak akiwa mahakamaniPicha: dapd

Kulingana na taarifa zilizotolewa na Televisheni ya Nile, Gamal Mubarak mtoto wa Mubarak aliyekuwa katika kamati maalumu ya Chama kilichokuwa kinatawala wakati huo na aliyetazamwa kama mrithi wa baba yake alitoa maamuzi mengi. Huku mtoto mkubwa wa kiongozi huyo Alaa aliyekuwa kando ya ulingo wa siasa akituhumiwa kwa kujihusisha mno na utesaji wa watu kadhaa, wakati wa utawala wa baba yake.

Watoto hawa wakiwa rumande katika gereza moja jijini Cairo wanasubiri hukumu yao jumamosi hii sambamba na baba yao mwenye umri wa miaka 84 anayezuiliwa katika hospitali moja ya kijeshi anakotibiwa ugonjwa wa moyo.

Ushahidi hauna dalili za kumtia hatiani

Wakati wa kesi yao kulikuawa na haliya mashahidi kujikanganya ambapo miongoni mwao ni Mkuu wa Jeshi la Misri na mtawala wa sasa wa Kijeshi Field Marshal Hussein Tantawi ambaye alitoa ushahidi faraghani. Kumekuwa na madai kuwa ushahidi mwingi uliotolewa hauna dalili za kumtia hatiani kiongozi huyo.

Tuhuma zingine zinazomkabili kiongozi huyo ni kitendo chake cha kuiuzia Israel gesi na kwamba alipokea rushwa kutoka kwa mfanyabiashara Hussein Salem.

Wakati kesi ikisikilizwa katika mahakama ya kijeshi nao Wamisri walitilia shaka kuwa kunaweza kukawa na upendeleo lakini mahakama hiyo imesema inafanya kazi bila ya kuingiliwa na ni mahakama huru lakini kesi hiyo ilianza kusikilizwa baada ya miezi kadhaa ya maandamano kuutaka utawala wa kijeshi kumfikisha mahakamani kiongozi huyo.

Mubarak anusurika kuuwawa mara kumi

Viongozi saba kutoka vyombo vya usalama, akiwemo Waziri wa mambo ya ndani wa Misri Habib al-Adly pamoja makamanda sita. Kwa wakati huu afya ya Hosni Mubarak aliyenusurika kuuawa mara 10 ni mbaya akisumbuliwa na ugonjwa wa moyo.

Mohammed Morsi, miongoni mwa wagombea wa nafasi ya Urais katika uchaguzi wa Juni 16 na 17
Mohammed Morsi, miongoni mwa wagombea wa nafasi ya Urais katika uchaguzi wa Juni 16 na 17Picha: picture-alliance/dpa

Miongoni mwa mtukio hayo ni mwaka1993 na jaribio jengine likafuata 1995 wakati gari lake lilipofyatuliwa risasi akiwa mjini Addis Ababa , Ethiopia alipokuwa akihudhuria mkutano wa viongozi wakuu wa nchi za kiafrika.

Mubarak alishika Uongozi wa Misri Oktoba 6, mwaka1981 mara baada ya kuuwawa kwa Rais wa pili Anwar Sadat aliyepigwa kupigwa risasi na wanamgambo wa kiislamu wenye misimamo mikali wakati wa gwaride la kijeshi.

Hukumu inayosubiriwa itakuja wakati Wamisri wanajiandaa na duru ya pili ya uchaguzi wa rais tarehe16 na 17 mwezi huu.

Wagombea wawili ni aliyewahi kuwa waziri Mkuu wa Mubarak Ahmed Shafiq aliyepata asilimia 23 na Mohammed Murs kutoka chama cha udugu wa Kiislamu, aliyeongoza duru ya kwanza kawa asilimia 24.

Mwandishi:Adeladius Makwega/AFPE

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman