1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HYDERABAD:Wafyatuaji bomu wasakwa na majeshi

26 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBVo

Majeshi ya usalama nchini India yananza kuwasaka waliofyatua mabomu mawili katika mji wa kusini wa Hyderabad yaliyosababisha vifo vya watu 40.Kulingana na maafisa wa polisi shambulio hilo lilitekelezwa na wapiganaji wa kiislamu.

Zaidi ya watu wengine 50 walijeruhiwa katika milipuko hiyo ya jana jioni iliyotokea katika mkahawa mmoja uliojaa wateja na ukumbi wa tafrija.

Majeshi ya usalama yalishika doria katika mji mkuu wa jimbo la Andhra Pradesh ili kuzuia ghasia zilizo na misingi ya kikabila kutokea.Hakuna aliyekiri kutekeleza shambulio hilo mpaka sasa.

Polisi wanaripotiwa kuvumbua bomu jengine hapo jana katika ukumbi wa filamu na kulitegua kabla kulipuka.Wataalam wa uchunguzi aidha wanashirikishwa ili kufanikisha juhudi za kuwasaka wahalifu waliofyatua mabomu.Waziri wa mambo ya ndani Shivraj Patil anatarajiwa kuzuru mji wa Hayderabad baadaye hii leo.

Mkuu wa jimbo la Andhra Pradesh ametangaza kufidiwa kwa familia za waliofiliwa baada ya mkutano wa dharura wa baraza la mawaziri.Kila familia iliyofiliwa inatarajiwa kupewa dola alfu 12,200.

Milipuko huo inatokea miezi mitatu baada ysa watu 11 kuuawa katika shambulio jengine la bomu lililotokea kwenye msiki wa Mecca ulio maarufu.Mpaka sasa polisi bado hawajagundua waliosababisha shambulio hilo.