1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ibada maalum kwa waliokufa na Tsunami

26 Desemba 2007

---

https://p.dw.com/p/CgNh

BANDA ACHEH

Mapema leo hii waindonesia wamefanya ibada maalum katika makaburi ya pamoja kwenye mkoa wa Acheh kisiwani Sumatra kuwakumbuka jamaa zao waliokufa katika gharka ya Tsunami miaka mitatu iliyopita.

Wakati huohuo Maafisa wa serikali walifanya majaribio katika mifumo ya kutoa onyo la mapema iliyowekwa baada ya kutokea kwa gharka hiyo.Mawimbi makubwa ya Tsunami yalichochewa na tetemeko la chini ya bahari lililokuwa na kipimo cha richta 8.5.Zaidi ya watu laki mbili walikufa katika nchi 12 zilizokumbwa na janga hilo.Nusu ya idadi hiyo walikufa katika eneo la Banda ache. Watu 45 elfu walikufa nchini Sri-Lanka na India.Shughuli za kuijenga upya Banda Acheh inatarajiwa kukamilika katika kipindi cha mwaka mmoja ujao.