1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ibrahimovic kuondoka PSG

13 Mei 2016

Zlatan Ibrahimovich amethibitisha kuwa ataondoka klabu ya Paris Saint-Germain mwishoni mwa msimu huu, lakini mabingwa hao wa Ufaransa wamesema nyota huyo atarejea baadaye katika wadhifa wa usimamizi

https://p.dw.com/p/1IncU
Frankreich Fußballer Zlatan Ibrahimovic in Paris
Picha: picture-alliance/dpa/EPA/Y. Valat

Ibrahimovic aliandika jana kwenye twitter kuwa leo atacheza mchuano wake wa mwisho uwanjani Parc des Princes. Alisema na namnukuu “nilikuja kama mfalme, naondoka kama shujaa”. Hivyo basi tangazo hilo limemaliza uvumi w amuda mrefu kuwa angeurefusha mkataba wake na PSG baada ya msimu huu.

Kumekuwa na uvumi mwingi kuhusu anakoelekea mchezaji huyo wa mwenye umri wa miaka 34 aliyewahi kuvichezea vilabu vya Ajax, Juventus, Inter Milam, Barcelona na AC Milan. Amehusishwa na uhamisho wa ligi ya Primia ya England. Swali sasa ni wapi ataelekea na ni nani atakayejaza nafasi yake katika PSG? Kuna baadhi ya majina kama vile Cristiano Ronaldo wa Real Madrid na Neymar wa Barcelona.

John Terry aongezewa mkababa na Chelsea

Nahodha wa Chelsea John Terry, ambaye alihofia kuwa hatowahi tena kuichezea klabu hiyo, amepewa mkataba mpya wa mwaka mmoja. Hayo yamethibitishwa na klabu ya Chelsea. Kaimu kocha Guus Hiddink ambaye anaiandaa timu yake kupambana na Leicester katika mchuano wa mwisho wa msimu, amesema kuwa Terry mwenye umri wa miaka 35 ameukubali mkataba huo. Ameichezea Chelsea zaidi ya mechi 700 tangu alipojiunga nao mwaka wa 1998.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA
Mhariri: Mohammed Khelef