1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ICC yaishitaki Chad kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa

Othman Miraji14 Desemba 2011

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu mjini The Hague (ICC) imesema inaipeleka Chad mbele ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kukataa kumkamata Rais wa Sudan, Omar Al Bashir, kwa mara ya pili.

https://p.dw.com/p/13SYR
Mahakama ya kimataifa ya kushughulikia kesi za uhalifu wa kivita iliyoko The Hague Uholanzi imesema inaiwasilisha Chad mbele ya baraza la usalama la umoja wa mataifa kwa kukataa kumkamata rais wa Sudan Omar Al Bashir kwa mara ya pili.
Rais Idris Deby wa Chad (kushoto) akimkaribisha Rais Omar el-Bashir wa Sudan.Picha: AP

Mahakama imetoa waranti wa kukamatwa kwa rais huyo wa Sudan anayetakikakana kwa madai matatu, ya mauaji ya halaiki, uhalifu dhidi ya binadaamu na uhalifu wa kivita uliofanyawa katika jimbo la Darfur. ICC imeliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuwa Chad ilikataa kumkamata Bashir alipoizuru nchi hiyo kati ya tarehe 7 na 8 Agosti 2011. Malawi pia imewasilishwa katika baraza hilo kwa kushindwa kumkamata rais huyo wa Sudan wakati alipokuwepo nchini humo.

Awamu ya pili ya uchaguzi wa Bunge yafanyika Misri

Sehemu ya pili ya uchaguzi wa bunge imeanza, ambapo mara hii wapiga kura milioni 18.8 katika mikoa tisa wanatakiwa kupiga kura hadi kesho (15.12.2011) jioni. Vituo vya kupiga kura mara hii vimefunguliwa huko Giza, Suez na Assuan.

Wapiga kura wakiwa kwenye foleni nchini Misri
Wapiga kura wakiwa kwenye foleni nchini MisriPicha: dapd

Hatua ya kwanza ya uchaguzi huo ilifanyika mwisho wa Novemba katika miji ya Cairo, Alexandria na mikoa mingine saba. Katika sehemu hizo, chama cha Udugu wa Kiislamu kilikamata nafasi ya kwanza, kikifuatiwa na chama cha siasa kali za Kiislamu. Watetezi wa mrengo wa shoto na waliberali waliambulia viti vichache.

Hatua ya tatu ya uchaguzi huo katika mikoa iliobakia itaanza Januari 3. Uchaguzi huu unafuatilizwa na mabishano kuhusu serikali ya mpito iliowekwa madarakani na Baraza Kuu la Kijeshi la Misri, na ambayo inakataliwa na baadhi ya makundi ya kisiasa.

'Umkhonto Wesizwe' latimiza miaka 50

Lililokuwa jeshi la wapiganaji wa chama cha ANC nchini Afrika Kusini wakati wa vita vya ukombozi, litaadhimisha miaka 50 Ijumaa ijayo, huku wapiganaji wa zamani wakiwa bado wanapigania kutambuliwa na serikali waliyoisaidia kuchukuwa madaraka.

Kamanda mkuu wa 'Umkhonto Wesizwe', Nelson Mandela.
Kamanda mkuu wa 'Umkhonto Wesizwe', Nelson Mandela.Picha: DW/AP

Jeshi hilo, UMKHONTO WEZISWE, yaani Mkuki wa Taifa, lililoundwa kupambana na utawala wa kibaguzi lilikuwa uti wa mgongo wa vita vya ukombozi. Jeshi hilo lililokuwa marufu kwa jina la MK lilikuwa na kambi za siri za mafunzo katika nchi kadhaa za Kiafrika na Urusi ya zamani.

Harakati za tawi hilo la kijeshi la chama cha ANC zilisimamishwa na kamanda wake wa kwanza, Nelson Mandela, baada ya kutoka gerezani mwaka 1990.