1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ICC yatoa waranti mpya dhidi Ntaganda

14 Julai 2012

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu imetoa waranti wa kukamatwa dhidi ya viongozi wawili waasi nchini Congo na Rwanda ambapo nchi hizo mbili zinashutumiana kwa kuwatumia kama mawakala wa vita katika ardhi ya Congo.

https://p.dw.com/p/15XgO
FILE- In this June 30, 2010 file photo, Congolese former warlord Bosco Ntaganda in his national army uniform attends the 50th anniversary celebration of Congo's independence in Goma in eastern Congo. In a marked turnaround, Congo's president Joseph Kabila called Wednesday, April 11, 2012 for the arrest of Ntaganda, a notorious ex-warlord and army general, who has been allowed to walk freely despite an international indictment, an official said. Ntaganda is accused of using child soldiers for fighting in Ituri, in northeastern Congo, from 2002 to 2003. (Foto:Alain Wandimoyi, File/AP/dapd) +++Abweichende Namen: Tanganda, Ntanganda, Ntangana, Ntagenda, Baganda, Taganda
Kiongozi wa waasi wa M23 Jean Bosco NtagandaPicha: dapd

Mahakama pekee ya kudumu duniani inayowahukumu wahalifu wa kivita , iliyo na makao yake makuu mjini The Hague, imetangaza kuwa imetoa waranti dhidi ya Sylvestre Mudacumura, kiongozi wa waasi wa Kihutu kutoka Rwanda anayeishi katika jamhuri ya kidemokrasi ya Congo.

Pia imetoa waranti mpya wa kukamatwa Bosco Ntaganda, jenerali laghai wa Kitutsi raia wa Congo , ambaye amepewa jina la utani , "Mharibifu", ambaye ameanzisha uasi unaoendelea sasa katika eneo la mashariki ya nchi hiyo akilitumia kundi linalofahamika kama M23.

Serikali zashutumiana

Serikali mjini Kinshasa inaishutumu Rwanda kwa kutoa fedha kwa kundi hilo, pamoja na silaha na vikosi vya jeshi kuwasaidia wanamgambo wa Ntanganda, ambao wamekamata miji kadha katika jimbo la Kivu ya kaskazini katika siku za hivi karibuni na sasa linaonekana kuwa linatishia kuukamata mji mkuu wa jimbo hilo Goma.

Congolese government soldiers prepare to drive from a military outpost between Kachiru village and Mbuzi hill, in eastern Democratic Republic of the Congo, May 25, 2012. Rival armed groups in Congo's eastern provinces are targeting each other's families, killing children, women and the elderly in some of the country's worst violence in years, officials said on Friday. The fighting, which UN agency UNICEF says has cost up to 80 lives since early May, comes amid a security vacuum in parts of the vast forested region after Congo's army redeployed elsewhere to capture a renegade general, Bosco Ntaganda, and his men. REUTERS/Siegfried Modola (DEMOCRATIC REPUBLIC OF CONGO - Tags: CIVIL UNREST MILITARY SOCIETY)
Wanajeshi wa jeshi la Congo wakiwasaka waasi wa M23 na kiongozi wao Bosco NtagandaPicha: Reuters

Ntaganda , ambaye ana umri wa karibu miaka 41, anatuhumiwa kufanya uhalifu wa kivita pamoja na uhalifu dhidi ya ubinadamu, kuanzia Septemba mosi mwaka 2002 hadi mwishoni mwa Septemba 2003, katika muktadha wa mzozo katika eneo la Kivu, imesema mahakama hiyo ya ICC.

Mahakama hiyo tayari ilishatoa waranti dhidi ya mbabe huyo wa kivita mwaka 2006 kwa kuwatumia watoto katika jeshi lake lakini katika mwezi wa Mei iliongeza mashtaka mengine.

Mahakama ya ICC imesema kuwa Ntaganda anadaiwa kubeba jukumu la mashtaka matatu ya uhalifu dhidi ya ubinadamu na manne ya uhalifu wa kivita, ikiwa ni pamoja na mauaji , ubakaji na utumwa wa ngono , mateso na uporaji na utekaji nyara.

Mzaliwa wa Rwanda

Ntaganda alizaliwa nchini Rwanda na alikuwamo katika jeshi la Rwandan Patriotic Forces, lililokuwa linaongozwa na rais wa sasa Paul Kagame, ambalo lilimaliza mauaji ya kimbari mwaka 1994 yaliyofanywa na Wahutu wenye msimamo mkali dhidi ya Watutsi walio wachache nchini Rwanda.

Wataalamu wanasema kuwa Ntaganda , ambaye alijumuishwa katika jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo pamoja na kundi lake la waasi wa Kitutsi katika makubaliano yaliyoshindwa ya mwaka 2009, alijitoa katika jeshi hilo Aprili mwaka huu wakati serikali mjini Kinshasa ilipokiondoa kikosi chake kutoka katika maeneo yenye utajiri mkubwa wa madini.

Serikali ya Kinshasa na ripoti ya wataalamu wa umoja wa mataifa inasema kuwa kuna ushahidi mkubwa wa ushiriki wa Rwanda katika uasi wa kundi la M23, dai ambalo Rwanda inakana.

Refugees from the Democratic Republic of Congo construct makeshift shelters at a refugee camp at Bunagana near Kisoro town 521km (312 miles) southwest of Uganda capital Kampala, May 15, 2012. The refugees fled the Masisi region in Congo's North Kivu province since fighting broke out between Congolese troops and fighters loyal to a renegade general Bosco Ntaganda. Clashes erupted after Congolese President Joseph Kabila announced last month he would try to arrest renegade General Ntaganda, wanted by the International Criminal Court (ICC) for war crime in northeastern Congo's ethnic conflict. Picture taken May 15, 2012. REUTERS/James Akena (UGANDA - Tags: SOCIETY CIVIL UNREST POLITICS)
Wakimbizi waliokimbia makaazi yao nchini CongoPicha: Reuters

Umoja wa mataifa na viongozi wa eneo hilo wamewataka viongozi wa Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kukaa chini na kufikia makubaliano ambayo yatazuwia kuongezeka kwa vita hivyo katika eneo la Kivu ya kaskazini ambalo tayari limeathirika kwa vita, ambapo vita vya hivi sasa vemesababisha mamia kwa maelfu ya watu kukimbia makaazi yao.

Mahakama ya ICC ilikataa ombi la kwanza la kutoa waranti dhidi ya kukamatwa kwa Mudacumura mwezi Mei lakini hatimaye mahakama hiyo ilitoa waranti siku ya Ijumaa, wakati mbinyo ukizidi katika pande zote mbili kwa ajili ya kufikia suluhisho la kidiplomasia katika mzozo huo wa Kivu.

Mwandishi : Sekione Kitojo / afpe

Mhariri : Idd Ssesanga