1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiDjibouti

Idadi ya waliofariki katika ajali ya boti Djibouti imepanda

Tatu Karema
25 Aprili 2024

Haya ni kulingana na Shirika la Uhamiaji la Umoja wa Mataifa IOM, ambalo limeangazia ongezeko kubwa la idadi ya watu wanaorejea kutoka Yemen kuelekea nchini humo mwaka huu.

https://p.dw.com/p/4fB8I
Pwani ya Djibouti
Pwani ya DjiboutiPicha: Sean Gallup/Getty Images

Ajali hiyo ya Jumatatu ni ya pili mbaya ya baharini katika muda wa wiki mbili katika nchi hiyo iliyoko kwenye kile kinachojulikana kama Njia ya Uhamiaji ya Mashariki kutoka Afrika hadi Rasi ya Arabia.

Katika taarifa hapo jana jioni, IOM imesema kuwa takriban watu 24, walifariki dunia na wengine 20 hawajulikani walipo baada ya boti iliyokuwa imewabeba wahamiaji 77 wakiwemo watoto, kuzama  karibu na mji wa Obock

IOM imesema kuwa manusura 33 wanaendelea kupata huduma katika kituo cha IOM mjini humo  Obock na kwamba maafisa wa eneo hilo wanaendelea kuwaendeleza juhudi za uokoaji kwa matumaini ya kuwapata manusura zaidi.