Idadi ya Wamisri waliojitokeza kupiga kura ni ya juu kabisa
3 Desemba 2011Matangazo
Chama cha Udugu wa Kiislamu na hasimu wake, chama cha kihafidhina cha Salafi, vina uwezekano mkubwa wa kupata wingi wa kura. Lakini kuna wasiwasi wa athari za serikali yenye msimamo mkali wa Kiislamu kwa uhuru binafsi wa watu, na kwa uchumi wa Misri unaoongozwa na utalii. Uchaguzi wa wabunge unafanywa kwa awamu tatu tafauti, ambapo utakamilika mwezi Machi mwakani kabla ya kufanyika uchaguzi wa rais katikati ya mwaka ujao. Baraza la Kijeshi, lililoingia madarakani baada ya Hosni Mubarak kutimuliwa, limeahidi kuwa hadi kufikia mwezi Julai mwakani litakuwa limeshakabidhi serikali kwa utawala wa kiraia.