1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iddi Ssessanga

10 Februari 2017

Mfahamu Iddi Sssessanga, mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW.

https://p.dw.com/p/2Wo5W
DW Kiswahili | Iddi Ssessanga
Picha: DW/L. Richardson
  1. Nchi ninayotokea: Uganda
     
  2. Mwaka nilipojiunga na DW: 2012
     
  3. Nilivyojiunga na DW: Nilikuja kama mkufunzi kwa miezi sita na kabla ya mafunzo nikaajiriwa
     
  4. Kwanini niliamua kuwa mwandishi wa habari: Kwa sababu sikutaka kuwa mwanasheria.
     
  5. Vigezo mtu anavyotakiwa kuwa navyo kuwa mwandishi wa habari: Mbali ya kuhitaji elimu stahiki, mtu anatakiwa awe na shauku ya kujua mambo mengi kadiri awezavyo kitaifa na kimataifa, amudu angalau lugha tatu za kimataifa. Awe tayari kutafiti kila anachotaka kuwasilisha kwa hadhira yake.
     
  6. Changamoto ninazokutana nazo kwenye maisha yangu ya kazi: Kuibuka kwa teknolojia mpya za habari na mawasiliano kila uchao.
     
  7. Tukio la kihistoria ambalo sitalisahau: Kuchaguliwa kwa Barack Obama kuwa rais wa Marekani mwaka 2008.
     
  8. Mtu ambaye ningependa kumhoji: Jakaya Mrisho Kikwete