1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

INSTANBUL : Iraq kuwashughulikia waasi wa Kikurdi

3 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/C7AF

Waziri Mkuu wa Iraq Nuri al-Maliki leo ameahidi kushirikiana na Uturuki katika mapambano yake dhidi ya waasi wa Kikurdi walioko kaskazini mwa Iraq kwa kusema kwamba serikali yake itachukuwa hatua kali zaidi dhidi ya Wakurdi hao wa chama cha PKK.

Maliki ameuambia mkutano na nchi jirani za Iraq na mataifa makubwa kwamba wamepitisha uamuzi wa kuyafunga makambi ya PKK kaskazini mwa Iraq.

Waziri Mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ameuambia mkutano huo kwamba hali hiyo inahitaji hatua ya haraka.