1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Inter Milan yatwaa ubingwa Ulaya mbele ya Bayern Munich

Aboubakary Jumaa Liongo22 Mei 2010

Mabao mawili ya Diego Milito katika dakika ya 35 na 70 yameipatia ubingwa wa kandanda kwa vilabu bingwa barani Ulaya Inter Milan ya Italia dhidi ya Bayern Munich ya Ujerumani katika fainali ya kusisimua mjini Madrid

https://p.dw.com/p/NV1w
Diego Milito wa Inter Milan akishangilia moja kati ya mabao yake mawili aliyofungaPicha: AP

Ni ushidini ambapo umezidi kumyanyua katika chati kocha wa timu hiyo mreno Jose Morinhno.Hii ni mara ya pili kwa Morinho kushinda ubingwa upingwa huo mara ya kwanza akiwa na FC Porto ya Ureno, kabla ya kuchukuliwa na Chelsea ya Uingereza.

Pamoja na kufungwa, lakini Bayern ilionesha mchezo wa hali ya juu ya kumiliki mpitra muda mwingi kuliko wapinzani wao.Arjen Robben alionekana kuwa mwiba  katika ngome ya Inter Milan iliyokuwa chini ya beki wa zamani wa Bayern mbrazil Lucio.Lakini ngome ya Bayern ilionekana kutokuwa makini na kutoa mwanya kwa Milito kupachika mabao hayo mawili.

Bayern ilipiga hodi mara nyingi zaidi katika lango la Inter lakini ilikuwa vigumu lango hilo kufunguliwa.Inter walipata nafasi nne ambapo mbili walizitumia kupachika mabao hayo na hivyo kuchukua vikombe vitatu katika msimu mmoja.

Inter Milan wametwaa ubingwa wa ligi ya daraja la kwanza Italia na kombe la chama cha soka nchini humo, kabla ya kutwaa uchampion wa Ulaya.

Jose Morinho amethibitisha umwamba wake katika kufundisha mbinu za kabumbu dimbani na hakuna shaka kuwa ni kocha bora duniani.

Nchini Ujerumani, miji yote ilikuwa kimya, huku washabiki wakirejea nyumbani mapema, na sherehe zilizoandaliwa zilivunjika

Mwandishi.Aboubakary Liongo