1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Irak na Uturuki kuimarisha ushirikiano wao

8 Machi 2008
https://p.dw.com/p/DL06

ANKARA:

Rais wa Irak Jalal Talabani amesema,nchi yake inataka kuwa na uhusiano imara pamoja na Uturuki.Talabani mwenye asili ya Kikurdi alipozungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara yake nchini Uturuki alisema,Irak inataka ushirikiano utakaokuwa mfano katika kanda hiyo.

Kwa upande mwingine,rais mwenzake wa Uturuki Abdullah Gul akizingatia kambi ya chama cha Kikurd cha PKK kaskazini mwa Irak alisema,nchi hizo mbili vile vile zishirikiane zaidi kupiga vita ugaidi.Vikosi vya Uturuki vilisitisha mashambulizi yake dhidi ya vituo vya PKK kaskazini mwa Irak,baada ya kuonywa mara kadhaa na Marekani kusitisha operesheni hiyo kwa haraka.