1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Irak yajadiliana na Uingereza kuhusu majeshi yake.

19 Oktoba 2008
https://p.dw.com/p/Fd0b

Baghdad:

Waziri mkuu wa Irak Nuri al-Maliki amesema kwamba nchi yake na Uingereza zimeanza majadaliano juu ya mkataba wa usalama ,kuamua hali ya baadae ya majeshi ya Uingereza nchini mwake baada ya mwaka huu 2008. Bw al-Maliki alisema katika taariafa iliotolewa na ofisi yake baada ya mazunguzmzo na Waziri wa ulinzi wa Uingereza John Hutton mjini baghdad leo kwamba Irak itateuwa ujumbe utakaojadiliana na Uingereza kuhusu suala hilo. Muda wa kuweko majeshi ya kimataifa nchini Irak ulioidhinishwa na Umoja wa mataifa unamalizika mwishoni mwa mwaka huu. Uingereza ina karibu wanajeshi 4.000 nkatika kambi moja nje ya mji wa kusini wa Basra.