1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran haitoyumbishwa na nchi za magharibi

4 Mei 2008

-

https://p.dw.com/p/DtL5

TEHRAN

Kiongozi wa juu nchini Iran amesema nchi hiyo haitayumbishwa kufuata haki zake na shinikizo za nchi za magharibi.Ayatollah Ali Khamenei ametoa matamshi hayo ikiwa nis iku mbili baada ya nchi zenye nguvu kusema kwamba zitatoa pendekezo jipya kuishawishi Iran kukomesha mipango yake ya kinuklia.Khamenei amesema Iran itaendelea na azma yake bila ya uoga na haitorudi nyuma na kwamba hakuna kitisho kitakachoishawishi nchi hiyo kugeuza msimamo wake.Ijumaa nchi zenye nguvu zilikutana mjini London Uingereza na kusema kwamba zitatoa mapendekezo mapya kwa Iran ili nchi hiyo iachane na shughuli zake za kurutubisha madini ya Uranium.Iran ambayo inasema mpango wake ni kwa ajili ya matumizi ya amani ilikataa mapendekezo ya awali ya nchi hizo za magharibi mwaka 2006.Nchi za magharibi zimekuwa zikiitaka Iran isimamishe mpango wake wa Kinuklia na badala yake kuisadia nchi hiyo kibiashara na vishawishi vingine.