1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran yaishutumu Marekani

10 Machi 2015

Serikali ya Iran imesema barua ya wabunge wa chama cha Republican cha Marekani kuhusu mpango wake wa nyuklia inaelezea tabia ya kutoaminika katika masuala fulani.

https://p.dw.com/p/1EoG4
Iran USA Kerry mit Sarif in Montreux
Mawaziri wa Mambo ya nchi za Nje wa Marekani na Iran, Jonh Kerry na Javad ZarifPicha: picture-alliance/AP Photo/E. Vucci

Serikali ya Iran imesema barua ya wabunge wa chama cha Republican cha Marekani kuhusu mpango wake wa nyuklia inaelezea tabia ya kutoaminika katika masuala fulani.

Waziri wa mambo ya nje wa Iran amesema barua kutoka kwa wabunge wa chama cha Republican nchini Marekani inayoonya kwamba makubaliano yoyote kuhusu mpango wa nyuklia yatatupiliwa mbali wakati rais Baracka Obama akiondoka madarakani inadhihirisha kwamba Marekani sio taifa la kuaminika.

Mohammed Javad Zarif amenukuliwa na tovuti ya televisheni ya Iran akisema barua hiyo ya maseneta 47 hakijuwa ya kidiplomasia na kwamba awali aliipuuza barua hiyo kwa kuona kama njama za propaganda za kisiasa.

Taarifa ya Ikulu ya Marekani

Ikulu ya Marekani na chama cha Demokrat vilevile imeikemea vikali barua hiyo, kwa kusema hatua hiyo ni kuhujumu mapatano yaliyopo. Marekani pamoja na mataifa mengine matano yenye nguvu duniani, yana matumani kwamba mpango kazi wa makabiliano utafikiwa mwezi huu na mapatano ya mwisho kufikiwa baadae mwaka huu, itadhibiti mpango wa nyuklia wa Iran kwa makubalino ya kuliondoshea taifa hilo vikwazo.

Washington Obama PK
Rais Barack Obama wa MarekaniPicha: Reuters/K. Lamarque

Makamo wa rais wa Marekani Joe Biden amesema hatua hiyo inamdhoofisha rais na kukwepa utelezaji wa mfumo wa kikatiba wa taifa hilo.

Kitisho kwa Iran

Katika barua ya wazi kwa viongozi wa Iran, maseneta wa chama cha Reblican kuonya kwamba makubaliano yoyote kuhusu mpango ya wa Iran na serikali ya Obama, utafikia kikomo pale ambapo rais Obama ataipa kisogo Ikulu ya Marekani.

Barua hiyo kali inatoa jaribio gumu kwa Obama na mataifa mengine matano kufanikisha makubaliano ya mwisho mwishoni mwa mwezi huu, yenye lengo la kufikisha mwisho mpango tata wa nyuklia wa Iran, ambao Iran yenyewe imekuwa ikisema mpango huo una malengo la ya amani au maendeleo ya taifa hilo.

Chanzo za taarifa kali

Hatua ya Republican inatekelezwa siku chache baada ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamini Netanyahu kuzungumza katika mkutano wake na Bunge la Marekani, baada ya kualikwa na spika wa bunge hilo kutoka chama cha Republican John Boehner.

Katika hotuba yake hiyo kwa wabunge Netanyahu alionya vikali kwamba mpango wa Marekani katika suala la nyuklia ya Iran utafungua njia ya Iran kufanikisha utengenezaji wa bomu.

Barua hiyo iliyoandikwa na seneta Tom Cotton aliye katika mhula wake wa kwanza , ilipelekwa kwa mara ya kwanza kinyume na katiba ya taifa hilo kwa lilionekana kama hasimu kwa Marekani.

Mwandishi: Sudi Mnette APE
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman