1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran yaonywa na Marekani kuwekewa vikwazo vikali

Martin,Prema/zpr14 Oktoba 2011

Rais Barack Obama wa Marekani ameonya kuiwekea Iran vikwazo vikali kabisa kutokana na madai ya kuhusika katika njama ya kumuua balozi wa Saudi Arabia nchini Marekani.

https://p.dw.com/p/RqpU
President Barack Obama gestures while speaking in the Rose Garden of the White House in Washington, Monday, Sept. 19, 2011. (Foto:Evan Vucci/AP/dapd)
Rais Barack Obama wa MarekaniPicha: dapd

Akizungumza mjini Washington, Obama alisema, hatua itakayochukuliwa na Marekani italenga kuitenga zaidi Iran. Hata kama viongozi katika ngazi za juu hawakuarifiwa kuhusu mpango huo, kuna suala la kuwajibika. Wakati huo huo, Obama amewalaumu waakilishi wa serikali ya Iran kuiongoza njama hiyo.

Hapo awali wajumbe wa serikali ya Marekani walikiri kuwa Marekani haina ushahidi thabiti kwamba viongozi wa ngazi za juu serikalini Iran, walikuwa na habari kuhusu njama hiyo. Iran inapinga lawama za kupanga kumuua balozi wa Saudi Arabia na imeituhumu Marekani kuwa inachochea vita.