1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran yapuuzia muda uliowekwa na Umoja wa Mataifa

Kabogo Grace Patricia23 Desemba 2009

Umoja wa Mataifa uliipa Iran muda wa hadi mwezi Desemba kusitisha mpango wake wa nyuklia.

https://p.dw.com/p/LB7z
Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Iran.Picha: AP

Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Iran amepuuzia muda wa mwisho uliowekwa na Umoja wa Mataifa wa nchi hiyo kusitisha shughuli zake za kinyuklia ama iwe katika hatari ya kuwekewa vikwazo zaidi.

Pendekezo la Umoja wa Mataifa linaitaka Iran kupeleka sehemu ya madini yake ya uranium ya kiwango cha chini nje ya nchi hiyo kwa ajili kurutubishwa zaidi.

Msemaji wa Ikulu ya Marekani-White House, Robert Gibbs amesema kuwa jumuiya ya kimataifa ilikuwa ikiuchukulia muda uliowekwa kwa umakini, hata kama Rais Ahmadinejad hakufanya hivyo.

Gibbs amesema kuwa nchi wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa pamoja na Ujerumani, watalishughulikia suala hilo ipasavyo.

Iran inasisitiza kuwa lengo la mpango wake wa nyuklia ni kwa ajili ya kuzalisha umeme ili uweze kuongeza zaidi gesi na mafuta.