1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran:Maelfu waudhuria mazishi ya Montazeri

21 Desemba 2009

Nchini Iran, maelfu ya waombelezaji, leo wameudhuria mazishi ya kiongozi wa ngazi ya juu wa kidini nchini humo,Ayatollah Hossein Ali Montazeri.

https://p.dw.com/p/L9pg
Ayatollah Hossein Ali MontazeriPicha: montazeri.com

Ayatollah Montazeri ambaye alikuwa mkosoaji mkubwa wa utawala wa sasa Rais Mahamoud Ahmednejadi, alifariki siku ya Jumamosi akiwa na umri wa miaka 87.

Kwa mujibu wa tovuti ya upinzani , maelfu ya waoambolezaji hao waliudhuria mazishi hayo  yaliyofanyika katika mji wa Qom.Hata hivyo hakuna chombo chochote cha nje kilichoweza kuthibitisha taarifa hizo kutokana na kuzuiwa na utawala wa Rais Ahmednejadi kufanya shughuli zao nchini humo.

Mideast_Iran_Montazeri_VAH103_441864921122009.jpg
Waombilezaji katika mazishi ya Ayatollah Hossein Ali MontazeriTPicha: AP

Lakini tovuti moja ya kikonservative iitwayo Asriran iliungana na ile ya upinzani ikisema kuwa idadi ya waombelezaji ilikuwa kubwa sana.

Ayotallah anachukuliwa kuwa mwanaharakati mkubwa wa haki za binaadamu, na ambaye pia alikuwa changamoto ya mabadiliko nchini Iran.

Viongozi wa upinzani nchini Iran Mir Hossein Mousavi and Mehdi Karroubi have waliitangaza siku ya leo kama ya maombolezi na kuwataka wafuasi wao kushiriki katika mazishi.

Kiongozi wa mkuu wa kidini wa Iran Ayotollah Ali Khamenei pamoja na kwamba Ayatollah Montazeri alikuwa mpizani wake, lakini ameitumia familia yake salam za rambi rambi.

Ayatollah Montazeri ilitegemewa angekuwa mrithi wa muasisi wa mapinduzi ya kiislam ya mwaka 1979, Ayatollah Ruhollah Khomeini ambapo alikuwa mmoja wa washiriki muhimu katika kuandaa katiba ya nchi hiyo.

Lakini kutoka na msimamo wake wa kuukosoa mfumo wa undeshaji nchi ikiwa ni pamoja na unyanyasaji dhidi ya wapinzani, Ayotollah Montazeri alilazimika kustaafu mnamo mwaka 1989 ikiwa ni miezi michache kabla ya kifo cha Ayatollah Khameini, ambapo aliambiwa na kiongozi huyo achane na masuala ya siasa.

Hata hivyo pamoja na onyo hilo Montazerii aliendelea kuwa mkosoaji mkubwa wa mfumo huo wa utawala  na alihoji umuhimu wa wadhifa wa Khomeini, hatua iliyomfanya  achukuliwe kama mhaini na mnamo mwaka 1997 aliwekwa katika kifungo cha nyumbani.

Miaka mitano baadaye aliachiwa huru kutoka na misingi ya afya yake kutokuwa nzuri, ambapo hata hivyo aliapa kuendelea kupinga na kutetea uhuru na haki.

Ayatollah Monatezerii alisimama hadharani kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu uliyomuweka kwa mara ya pili madarakani Rais Mahamoud Ahmednejadi, ikiwa ni pamoja na vitendo vya kuwapiga na kuwanyamazisha watu waliyoandamana kupinga uchaguzi huo.

" Kwani haki za wananchi zinakiukwaa, kwani uwagandamize watu wako, sielewi kwanini watu wafanyiwe hivi, kwa kigezo gani wanawapiga wanawake na wanaume´´

Mazishi ya kiongozi huyo wa juu ya kidini Ayatollah Montazerii yamefanyika katika mji mtakatifu wa Qom, ambapo waombelezaji wameendelea kuchukua nafasi hiyo kuandamana mitaani huku wakitamka maneno ya kuipinga serikali.

Tovuti moja nchini humo iitwayo Rahesabz imearifu kuwa katika mazishi hayo kulitokea tafrani miongoni mwa waombelezaji, pale wafuasi wa kundi la kihafidhina linaloiunga mkono serikali liitwalo Ansar Hezbollah, lilipojaribu kuwanyamazisha waombolezaji hao  waliyokuwa wakipaza sauti zao wakisema Montazeri hajafa ila ni serikali ndiyo iliyokufa.Anachukuliwa na wafuasi wake kama kiongozi mwenye mamlaka ya juu katika madhehebu ya kishia.

Mwandishi:Aboubakary Liongo/Reuters/AFP/ZPR    

Mhariri:Mohamed Abdul-Rahman