1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iraq ni mabingwa wa Kombe la Asia

Ramadhan Ali30 Julai 2007

Iraq jana ilitawazwa kwa mara ya kwanza mabingwa wa kombe la Asia baada ya kuizaba saudi Arabia katika finali bao 1:0.Ikawa shangwe na shamra,shamra kuanzia baghdad,Basra,kirkuk hadi Ulaya.

https://p.dw.com/p/CHbX
Alberto Contador-mshindi wa Tour de France
Alberto Contador-mshindi wa Tour de FrancePicha: AP

Jana ilikua “asie na mwana aeleke jiwe na asie na mguu alitia gongo” mkutano Baghdad,Basra na Kirkuk-nyumbani mwa wairaki wa madhehebu ya sunni,shiia na mwa wakurdi.Wote waliounganishwa pamoja na ushindi wa dimba wa kombe la bara la Asia,kitu ambacho hadi sasa wanasiasa walishindwa.

Kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Saudi Arabia katika finali ya Asian Cup mjini Jakarta, Iraq ilitawazwa kwa mara ya kwanza mabingwa wa kombe la asia lililoanzishwa 1956.Nahodha wao Yiunis Mahmoud aliufumania mlango wa Saudi mnamo dakika ya 71 ya mchezo kwa bao la kichwa na la ushindi –bao lililoasndika historia.

Kwa bao hilo,hakuna muiraki aliejizuwia iwapo ni mshia,msunni au mkurdi wote nchini Iraq na walikokimbilia,Jordan,Denmark,Sweden na Uingereza ilikua shamra-shamra:

Furaha ilioje kwa wairaki ambao baada ya maafa makubwa kwa mara ya kwanza wamepata kitu cha kufurahia,kitu cha kuwaunganisha-shetani wa dimba.Baada ya finali ya jana kumalizika, nahodha Mahmoud aliitaka Marekani kuondoa majeshi yake nchini Iraq,iondoke leo,kesho hata keshokutwa,lakini iondoke Iraqw.Akasema Mahmoud hatarejea Iraq na timu yake kusherehekea ushindi.Nikirudi na timu naweza nikauwawa au kujeruhiwa.

Iraq jana iliandika historia ya dimba,kwani ilitamba wakati madume wa Asia-Japan,Korea ya kusini,Iran na hataSaudi Arabia, walishindwa kuwika.Saudi Arabia,ilitaka kuwa timu ya kwanza kabisa kuvaa taji mara 4.hatahivyo, imefuta machozi kuona kombe la asia limeenda kwa nchi nyengine ya kiarabu.

Iraq ilishiriki mara moja tu katika kombe la dunia 1986.Na sasa itajiunga mwaka 2009 na Brazil,mabingwa wa dunia-Itali,Marekani,Oceania na wenyeji Afrika kusini katika kuania Confederations Cup-kobe la mashirikisho ikiwakilisha Asia na kufungua pazia la kombe la kwanza barani Afrika 2010,mwaka mmoja baadae.

Msangao mwengine katika dimba ni ushindi wa Botswana dhidi ya Angola,ilioshiriki mwaka jana katika kombe la dunia hapa Ujerumani.Katika finali ya jana ya duru za kwanza za kombe la COSAFA Castle Cup, mjini Gabarone, wenyeji Botswana waliikomea Angola mabao 3-1 kupitia changamoto za mikwaju ya penalty.

Timu zote 2 zilisimama suluhu 0:0 mwishoni mwa dakika 90 za kwanza.Huu ni mwaka wapili mfululizo

Kwa Botswana kuingia nusu-finali au timu 4 za mwisho.

Wanajiunga katika duru hiyo na Msumbiji,Bafana Bafana na mabingwa watetezi-Zambia.Mwaka jana Botswana ilizusha msangao kama huu katika hatua kama hii walipoipiga kumbo Afrika Kusini.

KOMBE LA DUNIA 2018 :

Franz Beckenbauer ,mwenyekiti wa kamati ya maandalio ya Kombe la dunia lililopita nchini Ujerumani na mjumbe katika halmashauri kuu-tendfaji ya FIFA,amependekeza kuwa kombe la dunia 2018 lianiwe nchini Uingereza.”hakuna nchi bora Ulaya kuandaa kombe la dunia 2018 kama Uingereza.Uingereza iko usoni kabisa.” Aliiambia Idhaa ya BBC.

Beckenbauer akasema jambo muhimu sana ni kuachana na ule mtindo wa zamu-kutoka bara hili kwenda jengine.Chini ya utaratibu wa rais wa sasa wa FIFA Sepp Blatter,kombe la dunia 2002 lilichezwa Asia-Korea ya kusini na Japan; lilile la 2006 likaaniwa Ulaya nchini Ujerumani na 2010 litahamia Afrika,likichezwa Afrika Kusini na baadae 2014 itakua zamu ya Amerika Kusini na yamkini ikawa Brazil,ilioandaa mara ya mwisho kombe hilo 1950.

Michezo ya pan American games, imemalizika jana mjini Rio de jeneiro,huku Brazil ikitamba jana kwa kunyakua medali 3 za dhahabu kati ya 4.Brazil mwishoe iliondoka na medali 161,54 kati ya hizo zikiwa za dhahabu-matokeo bora kabisa iliowahi kupata katika michezo hii.

Marekani ingawa jana haikupata medali,imeondoka ya kwanza kwa jumla ya medali 237 kati ya hizo 97 ni medali za dhahabu.Cuba ilifuata nafasi ya pili ikiwa imenyakua medali 59 za dhahabu na kufika hadi kumshinda hasimu yake Marekani katika mchezo wa baseball.

Ama katika mbio za baiskeli za Tour de France,

Zilizokumbwa na kashfa nyingi za madhambi ya doping-matumizi ya madawa kutunisha misuli na kuongeza kasi, zilimalizika jana kwa ushindi wa Mspain, Alberto Contador.Binafsi Contandor anatiliwa shaka kwa madhambi ya doping.