1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

IRBIL: Condoleezza Rice akutana na Barzani

6 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD5e

Waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani Condoleezza Rice amekutana na rais wa eneo la wakurdi nchini Irak, Ali Barzani. Siku chache zilizopita, utawala wa eneo hilo ulitishia kujitenga kutoka kwa Irak kwa sababu ya mzozo wa mafuta.

Bi Rice ametoa mwito kuwepo ushirikiano baina ya eneo hilo la Wakurdi na Irak, akisema fedha zinazotokana na uuzaji wa mafuta ni ufunguo muhimu utakaoleta uhuru wa kiuchumi na umoja wa Irak.

Barzani kwa upande wake amesema Kurdistan ina haki ya kujiendeleza lakini hata hivyo itaendelea kuunga mkono Irak yenye demokrasia. Condoleezza Rice amemshukuru Barzani kwa kushirikiana na Marekani na kushiriki katika juhudi za upatanisho wa kitaifa.

Hapo awali wakati wa mazungumzo yake na waziri mkuu wa Irak, Nuri al –maliki, mjini Baghdad, Bi Rice aliwashauri viongozi wa Irak waache elegevu wao wa kisiasa na wakomeshe machafuko ya kikabilia yanayoendelea nchini humo.