1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Isarel yashauriwa kuzungumza moja´kwa moja na Hamas

23 Februari 2008

-

https://p.dw.com/p/DCI3

JERUSALEM

Mkuu wa zamani wa usalama wa ndani wa Israel Yaakov Peri amesema hii leo kwamba Israel inabidi ianzishe mazungumzo ya ana kwa ana na kundi la Hamas juu ya masuala kama vile ubadilishanaji wa wafungwa na mashambulio ya roketi kutoka Gaza dhidi ya miji ya Israel.

Akizungumza na Redio ya Israel Yaakov amesema mazungumzo ya ana kwa ana baina ya pande hizo mbili ndio njia pekee inayoweza kuleta suluhisho la haraka katika mgogoro huo badala ya mashauriano kusimamiwa na Misri na mataifa mengine.Israel inajaribu kutafuta njia za kuachiwa huru kwa mwanajeshi wake aliyetekwa nyara na kundi la wanamgambo wanaohusiana na Hamas mnamo mwezi juni mwaka 2006 lakini taifa hilo la kiyahudi linapinga kuwa na mazungumzo ya ana kwa ana na Hamas.