1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ishara za kuivamia Anjouan huko Comoro zaanza

Kalyango Siraj12 Machi 2008

Majeshi ya serikali ya Comoros yawakamata wapiganaji wa Bakari katika kisiwa cha Nzuwani

https://p.dw.com/p/DNTK

Jeshi la Comoros limechuka mateka wapiganaji kadhaa wa kiogozi muasi wa kisiwa cha Nzuwani -Muhamed Bakari katika kile kinachoonekana kama mwanzo wa operesheni ya kukivamia kisiwa hicho.Wapiganaji hao walichukuliwa na majeshi ya Comoros kutoka kisiwa cha Nzuwani.

Vikosi vya jeshi la Comoro viliingia kwa mda na baadae kutoka katika kisiwa kilichoasi cha Nzuwani.

Kwa mda sasa, jeshi la comoro likisaidiwa na majeshi kutoka mataifa kadhaa ya Umoja wa Afrika yamekuwa yakijiiandaa kwa kukivamia kisiwa cha Nzuwani ili kuweka uawala wake kuwa chini ya serikali ya Comoro inayoongozwa na rais Ahmed Abdallah Sambi.

Kwa sasa kisiwa cha Nzuwani kiko mikononi mwa Muhamad Bakari aliejitangaza mtawala wa kisiwa hicho kwa mda sasa. Miito ya kumtaka kuachana na madai yake hayaikufaulu.

Radio ya taifa ya Comoro imetangaza kuwa majeshi yake yamewakamata hao wapiganaji wa Bakari, na hii kutoa ishara kuwa huenda ile operesheni ya majeshi imeanza.

Waziri wa Comoro wa elimu ya taifa na utafiti na pia msemaji wa serikali Abdulrahim Saidi Bakari akizungumza na Deustche Welle kwa simu kutoka Moroni,amefafanua hali halisi akisema majeshi yaliweza kujipenyeza tu jumanne katika kisiwa hicho na kuwakamata wanamgambo watatu lakini mtu wa nne ambae ndie aliekuwa kiongozi wao na mlengwa alitoroka.

Ameongeza kuwa watu waliokamatwa ni maafisa wa kundi la mgambo la Ahmed Bakari na kuongeza kuwa mtu wa nne,ambae ndie alikuwa kiongozi wao na ndie aliekuwa shabaha alitoroka kabla ya kukamatwa.

Ameongeza kuwa hatua yao hii ni kama onyo kwa wahusika kuwa hawawezi kuwazuia kwenda huko ikiwa watataka.

Wanajeshi kadhaa wamekusanyika katika kisiwa jirani cha Mwali wakisubiri amri pamoja na msada kutoka kwa umoja wa Afrika kutekeleza shabaha yao ya kukivamia kisiwa hicho.

Umoja wa Afrika, ukitaka kutakasa jina lake kutokana na kushinwa katika operesheni kadhaa barani Afrika kama vile Somalia na mkoa wa Sudan wa Darfur,umeahidi kutuma vikosi Comoro kuunga mkono serikali ya huko kuweza kufany hujuma katika kisiwa cha Nzuwani,kilicho na idadi ya watu wanaofikia laki tatu.

Majeshi ya Tanzania na Senegal yameanza kuwasili mjini Moroni,

Mkuu wa jeshi wa visiwa hivyo Kanali Mohamed Amiri Salimou amenukuliwa akisema kuwa jumla ya wanajeshi 500 wa Tanzania watakuwamo visiwani humo.

Majeshi hayo ya Afrika yanatarajiwa kuelekea katika kisiwa cha Mwali.

Afisa mmoja wa Serikali ya nchi hiyo amearifu kuwa wanajeshi 75 wa Senegal waliwasili mjini Moroni siku ya Jumatatu.

Sudan, Tanzania, Senegal na Libya ni nchi nne ambazo zimepewa mamlaka na Umoja wa Afrika kusaidia serikali ya Comoro katika juhudi za kujaribu kurudisha tena mamlaka ya serikali kuu katika kisiwa cha Nzuwani kutoka kwa Rais muasi Mohamad Bakari.

Comoro yenye idadi ya watu takriban laki saba imeshuhudia mapinduzi ya kijeshi pamoja na majaribio ya kijeshi 20 tangu ijipatie uhuru kutoka kwa Ufaransa mwaka wa 1975.

Nacho kisiwa cha Nzuwani kilijaribu kujitenga kutoka Comoro mwaka wa 1997 na maafisa wa Comoro wanasema kuwa Muhamed Bakari ambae alipewa mafunzo ya kijeshi na Ufaransa anataka kufanya hilo.