1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Islamabad. Afisa mwandamizi katika mahakama auwawa.

14 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC23

Nchini Pakistan , watu wenye silaha wamempiga risasi na kumuua afisa mwandamizi katika mahakama kuu ya Pakistan. Polisi wamesema kuwa wapiganaji kadha wamemuua Syed Hammad Raza mapema alfajiri leo nyumbani kwake mjini Islamabad.

Wakati huo huo , mgomo uliotishwa na vyama vya upinzani umesababisha mji wa Karachi pamoja na miji mingine kutokuwa na shughuli zozote.

Maduka na shule zimefungwa , na usafiri kwa umma kwa kiasi kikubwa haufanyikazi katika mji wa Karachi, mji ambao ni eneo la kibiashara upande wa mashariki ambako karibu watu 40 wameuwawa mwishoni mwa juma katika mapigano baina ya wale wanaoipinga na wale wanaoiunga mkono serikali.

Ghasia zimezuka siku ya Jumamosi baada ya wanaharakati wanaoiunga mkono serikali kumzuwia jaji mkuu Iftikhar Muhammad Chaudhry kuhutubia mkutano wa hadhara kufuatia kuachishwa kwake kazi mwezi wa March na rais Pervez Musharraf. Musharraf ameamua kufuta kazi Chaudhry kuhusiana na madai ambayo hayakuelezwa ambayo ni pamoja na kutofuata taratibu.