1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Islamabad. Bhutto achwa huru.

16 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CI1d

Maafisa nchini Pakistan wamemuacha huru kiongozi wa upinzani Benazir Bhutto kutoka kizuizi cha nyumbani , saa chache baada ya uteulizi wa waziri mkuu wa muda ikiwa ni hatua ya kwanza kuelekea uchaguzi mkuu. Maafisa wa magereza waliondoka kutoka katika nyumba ya Bhutto katika eneo la mashariki mjini Lahore ambako Bhuto amekuwa akizuiliwa ili asiweze kuongoza maandamano ya kudai demokrasia dhidi ya amri ya hali ya hatari iliyotolewa na rais jenerali Pervez Musharraf. Musharaf ameahidi kufanya uchaguzi mkuu nchini humo ifikapo tarehe 9 mwezi wa Januari na amemteua spika wa baraza la seneti Mohammadmian Soomro kama waziri mkuu wa muda. Wakati huo huo Bhutto na waziri mkuu wa zamani anayeishi uhamishoni Nawaz Sharif wameripotiwa kukubaliana kuunganisha nguvu zao kumuondoa rais Musharraf. Wakati huo huo Marekani imeonyesha kupotea kwa uvumilivu wake leo kwa kushindwa kwa rais Musharraf kuondoa sheria ya hali ya hatari na kujiuzulu kama kiongozi wa majeshi. Waziri wa ulinzi wa Marekani Robert Gates ameshauri kuwa uwezo wa rais Musharraf kama mshirika wa Marekani katika vita dhidi ya ugaidi unaingia shaka , na amesema anapaswa kuondoa amri ya hali ya hatari na kuondoka kutoka jeshi haraka iwezekanavyo.