1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD : Bhutto azuiliwa kukutana na jaji mkuu

10 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CBKA

Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan Benazir Bhutto leo amezuiliwa kukutana na baadhi ya mahakimu waandamizi waliotimuliwa kutoka Mahkama Kuu akiwemo Jaji Mkuu Iftikhar Chaudhry ambao wako katika vifungo vya nyumbani.

Kutimuliwa kwa mahakimu hao kwenye nyadhifa zao kumekuja baada ya Rais Pervez Musharraf kutangaza utawala wa hali ya hatari nchini Pakistan.

Bhutto mwenyewe hapo jana alikuwa kwenye kifungo cha nyumbani ambapo polisi waliizigira nyumba yake kwa kuiwekea vizuizi vya senyen’ge na kangriti kabla ya kuruhusiwa kutoka nje leo hii.

Kufuatia kuachiliwa kwake kutoka kifungo cha nyumbani cha siku nzima Bhutto pia leo amehutubia kundi la waandishi wa habari waliokuwa wakipinga kuwekewa vikwazo kwa vyombo vya habari.