1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Islamabad. Familia kadha zakimbia mapigano.

9 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7HB

Mamia ya familia yameanza kukimbia kutoka katika jimbo la kaskazini nchini Pakistan la Waziristan ambalo linapakana na Afghanistan. Hii inafuatia siku tatu za mapigano makali kati ya majeshi ya serikali ya Pakistan na wanamgambo wanaounga mkono Taliban , ambapo zaidi ya watu 150 wameuwawa. Jimbo la Waziristan linaonekana kuwa ngome kuu ya wagambo wa Taliban. Mapigano hayo ya hivi karibuni yanakuja baada ya wapiganaji kushambulia kwa kushtukiza mlolongo wa magari ya jeshi la Pakistan .