1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD : Hali ya hatari kuondolewa baada ya mwezi mmoja

Mohamed Dahman10 Novemba 2007

Afisa wa serikali ya Pakistan amesema kwamba utawala wa hali ya hatari uliowekwa nchini humo na Rais Pervez Musharraf yumkini ukaondolewa katika kipindi kisihozidi mwezi mmoja wakati waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo Benazir Bhutto akiwa ameaachiliwa kutoka kifungo cha nyumbani.

https://p.dw.com/p/CB0k
Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan Benazir Butto yuko huru tena kufuatia kifungo cha nyumbani cha siku nzima.
Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan Benazir Butto yuko huru tena kufuatia kifungo cha nyumbani cha siku nzima.Picha: AP

Musharraf ametetea utawala wa hali ya hatari kwa kusema kwamba Waislamu wa itikadi kali na kuingilia kati kwa mahkama katika shughuli za kuendesha nchi kutapelekea kujiuwa kwa Pakistan.

Waziri Mkuu wa zamani wa nchi hiyo Benazir Bhutto ameondoka nyumbani kwake mjini Islamabad leo hii baada ya kuwa kwenye kifungo cha nyumbani kwa siku nzima hapo jana ili kumzuwiya asihutubie maandamano katika mji wa karibu wa Rawalpindi kupinga utawala wa hali ya hatari.

Kulikuwa na ulinzi mkali wa polisi kwenye nyumba ya Bhutto hapo jana ambayo ilizingirwa kwa senyen’ge na vizuizi vyengine vya kangriti.

Sherry Rehman msemaji wa chama cha Bhutto cha PKK anasema chama kizima kimejitolea muhanga hapo kabla kwa ajili ya kurudisha demokrasia na wako tayari kufanya hivyo hivi sasa.Hawataki kumwaga damu katika mitaa ya Islamabad au Pakistan lakini wamefikishwa mahala ambapo hawana jinsi kwamba watapinga ukandamizaji huo kwa nguvu zao zote.

Amri ya kumzuwiya Bhutto nyumbani kwake iliondolewa hapo jana usiku na tayari ametoka nje ya nyumba yake leo hii kuelekea kwenye mikutano na maafisa wa chama chake,viongozi wa vyama vya kijamii na wanadiplomasia wa kigeni.