1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Islamabad. Jaji mkuu arejeshwa katika wadhifa wake.

21 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBgf

Mahakama kuu nchini Pakistan imemrejesha katika wadhifa wake jaji mkuu Iftikhar Chaudhry.

Majaji wamesema kuwa rais Pervez Musharraf ambaye amemsimamisha kazi Chaudhry March mwaka huu kwa madai ya utovu ya nidhamu ni kinyume cha sheria.

Jaji huyo amekuwa akidai kuwa kuachishwa kwake kazi kumehusika na masuala ya kisiasa.

Chaudhry amekuwa chachu ya upinzani dhidi ya utawala wa Musharraf.

Munir A Maliki ,rais wa chama cha wanasheria wa mahakama kuu na msaidizi wa jaji mkuu ameisifu hukumu hiyo.

Ilikuwa ni hukumu ya kihistoria. Tuliwaahidi watu wa Pakistan kuwa hatutaangalia athari za kesi hii kwa mtazamo wetu. Mzozo huu juu ya jaji mkuu ulianza kwa sababu utawala wa kidemokrasia ulipuuzwa. Na sasa awamu ya pili ni kupambana na kupata utawala wa raia.

Uamuzi huo unaonekana kuwa ni pigo kubwa kwa Musharraf ambaye ameitawala nchi hiyo bila kupata changamoto kubwa kwa muda wa miaka minane. Kurejeshwa kwa jaji huyo kunaweza kuleta hali ya matatizo kwa mipango ya rais huyo kwa ajili ya kuchaguliwa kwa kipindi kingine cha utawala katika miezi inayokuja.