1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD: Kamanda wa Taliban auwawa

25 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBfV

Polisi nchini Pakistan wamesema kamanda wa kundi la Taliban ameuwawa nje ya nyumba yake mjini Chaman.

Qari Naimatullah alishambuliwa na watu wawili waliokuwa wamejihami na bunduki na kuuwawa wakati alipokuwa akirejea nyumbani kutoka shule ya kiislamu alikokuwa akifundisha.

Wakati huo huo watu takriban saba wameuwawa na wengine 30 kujeruhiwa kwenye shambulio lililofanywa na wanamgambo wa kiislamu katika mji wa Bannu kaskazini magharibi mwa Pakistan.

Duru za polisi zinasema maroketi manne yamevurumishwa, mengine kwenye makaazi ya raia.

Mji wa Bannu ni njia ya kwenda katika eneo la Waziristan Kaskazini, linalopakana na Afghanistan, amblao limekuwa ngome ya wanamgambo walio na mafungbamano na kundi la al- Qaeda.

Katika miezi ya hivi karibuni wanamgambo hao wameongeza mashambulio yao baada ya kufutilia mbali mkataba wa kusitisha mapigano baina yao na serikali uliodumu kwa miezi kumi.